''We believe, life is only a gift that expires and success in anything we have is not ours, its for human kind and so our wisdom''
-Gwemela
JE? UNATAMANI KURUDIA ZAMANI.
Gwemela. 0674167126
Hivi kuna yeyote kati yetu anatamani kurudi kwenye zama za zamani alikopita hata kama kwa sasa hayuko imara...? basi ukiona unatamani maisha ya zamani na ulikuwa huko zamani huna maisha mazuri...mmmh umekosea kati ya hivi vitu.
1. Kuwa na imani potofu.
Yaani namaanisha kuamini vitu fulani ni vya watu fulani na havihusiani na wewe. wapo wanaoamini kuwa na utajiri ni kunaweza kukupeleka motoni.. lakini kama ukiiba kwa njaa au ukimsema jirani yako kwa yeye kula chakula kitamu alafu wewe huna utaishia pia na wewe motoni.
2. Kuacha kujituma na kuridhika na kidogo.
Ni msemo mkubwa sana kwenye jamii yetu ya sasa... "kuwa naridhika na kidogo nilicho nacho" nakukumbusha bure tu hapa "KILA KIDOGO CHA SIKU INAYOFUATA NI KIDOGO ZAIDI YA KILE CHA SIKU ILIYOTANGULIA" waingereza wanasema "Aim to the moon, if not to the moon it will fall to the stars"
yaani kifupi tunweza sema hapa "Aim higher" ikiwa na maana kuwa "Adhimia kupata kikubwa, ili ukikikosa utapata kikubwa kidogo" .
3. Kutokuwa na malengo ya wazi.
Walio wengi kama upo kwenye hilo kundi ambalo unatamani ungerudi nyuma basi jua aidha huna malengo kabisa au unayo ila yenye kukufanya ukamilishe salama siku yako.
Ipo hivi, ukiwa na malengo yako unataka yatimie.. tafadhali yape muda wa kuyatafakari kila jioni au asubh ya siku.
4. Kukaa na mawazo Mgando.
Kuwa na ratiba moja kila siku, kukaa na kundi la watu wa aina moja kila siku, kuwa na marafiki mgando ambao kila wakati wao hawawezi kukuboresha kimawazo na kimkakati.
We waepuke Mapema kama unaweza kuwaepuka.
5. Kila Wakati Muombe M/Mungu akupe Mafanikio.
Wengi wanaweza sema mbona tumeomba sana lakini Mungu hajajibu. Kiukweli Mungu anajibu kwa wakati wa mapema sana lakini sisi ndio hatuoni.
•Mungu ukimuomba hela anakupa nafasi ya kupata pesa na sio pesa halisi.
•Mungu ukimuuliza kazi, anakupa nafasi ya kupata kazi na sio kazi.
•Ukimuomba Afya, anakupa uelewa wa wewe kubaki na afya.
KIFUPI MUNGU ANAJIBU KWA KUKUPA NAFASI YAANI OPPORTUNITIES..
UNAWEZA KUBADILISHA MAISHA YAKO MAGUMU KUWA MAZURI...
MAAMUZI NI YAKO KUBAKI HIVYO ULIVYO AU KUFUATA HIZI KANUNI MUHIMU ZA MAFANIKIO.
*IKUMBUKWE ZIKO NYINGI ILA FACEBOOK NI MAHALI AMBAPO HUWEZI ANDIKA KILA KITU. NA KAMA KUNA MTU ATAPENDA NIAANDIKE KITABU KUHUSU KUINUKA KIUCHUMI BASI ANAWEZA NITUMIA MESEJI NIKAANDA KITABU HUKU NIKIKUSANYA KILA SIRI YA MUHIMU.
*PLEASE COMMENTS ZIWE NYINGI.
NIWASHUKURU BABA NA MAMA YANGU KWA KUNIFANYIA MAKUBWA YASIOELEZEKA NA PIA NDUGU ZANGU.