HOW MONEY CAN BE PUT INTO RIGHT USE IN 2020/2021

''We believe, life is only a gift that expires and success in anything we have is not ours, its for human kind and so our wisdom'' -Gwemela
SOMO LA KWANZA KUHUSU UCHUMI.

Jina: Gwemela Conrad Michael.
Elimu itolewayo: Ujasiriamali na uchumi.
Vitabu vya kuhakiki.
1. Rich dad poor dad by Robert kiyosaki.
2. The power of subconscious mind.
3. The Contagious
4. Art of war by Sitzu.

Mobile number: +255674167126
email gwemelaconrad@gmail.com

Youtube Channel: Brightermango
twitter/instagram: brightermango

Awali ya yote nimshukuru mwenyezi Mungu anayetupa uhai huu wa kila siku na kuturuhusu tuyajue yote tunayoyajua kwa sasa.

Pili; Nimshukuru Mama na Baba pamoja na familia yangu kwa ujumla kutokana na upendo wao wa dhati kwangu kwa kipindi chote cha maisha haya ya upendo wa kweli.

Tatu niswashukuru Marafiki na wapendwa wasomaji wa makala zangu hizi za elimu ya uchumi wa kujitegemea...

Hivyo ni matumaini yangu kuwa Kupitia ushirikiano na ushirikishwaji wa kila pande tutapiga hatua..

  *STORI_YA_ROBERT_KIYOSAKI*
Photo credit: Google


Robert kiyosaki Muandishi wa kitabu cha "Rich_dad_poor_dad" akiwa na umri wa miaka 9 aliwahi muuliza baba yake ambaye alikuwa na elimu ya juu Yaani Ph.D kuwa kwanini shuleni hawatoi elimu ya fedha...na baba yake alimjibu kuwa serikali haijaruhusu wakufunzi watoe elimu fedha...akamuuliiza tena kwanini basi yeye ameamua kufanya kazi ya serikali.... Baba akamjibu kuwa yeye anafanya kazi na alisoma ili afanye kazi serikalini na sio vinginevyo...baba yake akamwambia kuwa lakini asijali kwani yuko na rafiki ambaye pia naye kwake ni baba wa rafiki yake kipenzi aitwaye *Ema*.
Basi Robert akaamua kwenda kwa baba yake Ema na kumtaka awe mwalimu wake kuhusiana masuala ya fedha...
 sababu ya yeye kumuamini mzee yule kwenye masuala ya kifedha ni kwa sababu ya uzoefu wake kwenye nyanja hiyo..... Kwani alianza kujifunza kutoka kwa watu halisi wa kila kitu alichotaka kukifanya.

  ####*WALIMU HALISI NA WASIO*####

Baba yake Ema aliwapoteza wazazi wake akiwa na umri miaka 13 hivyo ilikuwa wazi ni pigo kwenye maisha yake na hivyo alijifunza karibuni kitu kutoka kwa walimu halisi yaani wale wanaofundisha vitu ambavyo wao pia wanafanya... kama vile Wahasibu na uhasibu pia kwa upande mwingine kujua mzunguko wa fedha kutoka kwa mtumiaji wa mwisho na muuzaji wa jumla na pia athari zitokanazo na ukwasi kubaki mahali pasipo na kuondoka.
... Pia alipata na nafasi ya kujua saikolojia iliyopo nyuma ya mafanikio ya kweli na utajiri au ukwasi wa kweli na tofauti kuu kati ya muajiriwa na mjasiriamali mwenye mafanikio ya wazi.
SOMO LA PILI KUHUSU UCHUMI.

Jina: Gwemela Conrad Michael.
Elimu: Ujasiriamali na uchumi.

Tembelea blog yangu brightermango.blogspot.com
na twitter/instagram brightermango

#*UKWELI TUNAOFICHWA KUHUSU UTAJIRI*#
Unajua?
Wachumi wengi wanatuficha maana hii ya uchumi ambayo hata wasomi huipuuuza sana lakini ni hii...
... UCHUMI NI kutumia mali chache ulizonazo kukidhi mahitaji/haja au mambo mengi yanayozihitaji hizo mali..
yaani kwa lugha ya kimombo ni kua .... "Economy Is study out of which man thinketh and use limited resource to satisfy unlimited needs"

Kwahiyo tukirejea kwa ndugu yetu Robert alikuwa akijifunza njia mojawapo ya kutumia mali chache ili kukidhi haja nyingi alizokuwanazo....alikuwa akijifunza "game monopoly" 
google credit.


Kwa kipindi chote ambacho Robert alikuwa yuko na Baba yake Ema alikuwa halipwi kiasi chochote cha fedha.. hii inamaanisha kuwa Robert alifanya kazi bure kwa mzee yule.
   Robert anaeleza kuwa Mzee yule alimruhusu afanye kazi chini yake ili ajifunze vitu muhimu kuhusu fedha na kujifunza kwake hakupaswa kulipwa... kwahivo hakulipwa chochote na mzee alimueleza kuwa tofauti kubwa kati ya mjasiriamali na mfanyakazi yeyote.... ya kuwa mjasiriamali ndie mmiliki wa huduma na hivyo hawezi kujilipa na ni kama mzee aliruhusu robert aijue siri hii lakini pili ni ile ya mfanyakazi kutumikishwa na kupewa mfumo shikamanifu yaani ule wa bima... huu mfumo ni wa kulemaza mtu asiwaze kujitunza kwani anajua mwajiri wake atashughulika na afya usafiri na mahitaji yoote yanayoshughulikiwa na bima... lakini siri ya tatu ni ile ya kuidhuru akili ya mtu maskini kwa kigezo kuwa yeye ni maskini milele na hivyo kutaka zaidi ni dhambi na anapaswa kushukuru kwa kipato kidogo alichonacho.
photo credit:Google.


  Haya Bwana Siku zikapita na Robert akawa haelewi chochote kwani alidhani elimu ya fedha angeipata darasani na badala yake akawa akifanyishwa kazi tena kwa mfululizo huku akishirikishwa katika kila kitu hasa kwa sera ya mzee Ya "game monopoly" 
  Hivyo Robert ilimbidi aulize swali muhimu ya kuwa ni lini wangeaza kusoma ... basi mzee akamuuliza hiki tunachofanya ni nini? Robert akajibu tunafanya "Game monopoly", mzee akamuuliza tena naye akajibu tunafanya "Game monopoly" basi mzee akauliza tena ...ikambidi Robert Kiyosaki ajibu kuwa Hajui chochote... basi mzee akasema nakufundisha elimu ya fedha...
 Baba Ema akajiegesha kwenye kitasa cha mlango na akasema My son tunachofanya hapa ni kweli kinaitwa "GAME MONOPOLY" Lakini pia hiki ndicho kinafanyika kwenye maisha halisi ya kila siku.

...Je? ROBERT KIYOSAKI alijifunza Nini.
itaendelea!

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post