MALIZA MWAKA KIPEKEE➿..HIZI HAPA TIPS💥💥

💥🔥DECEMBER TO REMEMBER🔥💥

JINA: GWEMELA CONRAD MICHAEL.
USERNAME: BRIGHTERMANGO.
WHATSAPP: +255674167126.

  Jana nimepitia kurasa ya MillardAyo, kwenye sehemu ya arafa(comments) nikakuta mtu ameandika hivi
"JANA NILITISHIA KUJIUA, LAKINI CHA AJABU MAMA AKAMWAMBIA DADA APUNGUZE MAJI YA UGALI, MMOJA HAYUPO"
Mwanzo nilicheka sana, ila baadae sana nikagundua kuna kitu hakipo sawa, maana yule mtu aliyeandika arafa ile hakuwa kajibu au kutoa maoni kwenye kurasa na chapisho lile la #millardayoupdates saa nikawazaa? ivi kwanini jamaa aliwaza kuandika alichokiandika.

📣MAMBO MATANO YA KUJIFUNZA KUTOKA KWENYE KAULI ILE TATA💥

   1. ACHA MARA MOJA KUWA TEGEMEZI KWA WAZAZI.

Yawezekana kabisa uko na haki ya wazazi, lakini sio haki ya wazazi wako maskini waliokufikisha miaka ishirini au thelathini kuendelea kukulea, Hebu fikiria kidogo madhara ya utegemezi wako. Yaweza kuwa wewe sio mwizi wala mdokozi, lakini kukwepa kwako majukumu ndio chanzo cha umaskini wenu... kwahiyo kwenye kauli inaelekea mzazi ameshakuchoka.

2. RUHUSU MAJADILIANO.
Yawezekana kijana aliyetoa taarifa ya kumshtua mama yake angegundua tu kuwa mama yake hana mpango nae, pale tu angemshaurisha kwa kupita pembeni, hapa namaanisha aghalabu angejaribu basi kuuliza ni vipi maamivu ya kumpoteza mtu aliyejinyonga yalivyo, kwani kwa kauli hii iliyopita, Jamaa hatajinyonga, lakini pia hatoendelea na upendo wa dhati,ila tu UPENDO wenye mashaka tele.

3. KWENYE MAISHA USIJARIBU KUSHTUA JIWE.
Ninachokimaanisha hapa ni kuwa, hata iweje kama unahangaika kushtua jiwe liinuke na kutembea basi unajisumbua, kutokana na kauli hii ya msingi, jifunze kutembea na vinavyoshtuka haijalishi ni wazazi au watu wako wa karibu, kama unagundua hawawezi kushtuka, basi hapo wamepoteza imani na kamwe hawataweza kukusaidia pindi tu utakapoingia kwenye shida.



4. USIJALI KUHUSU WANAOKUZUNGUKA.

Hofu ya kufanya mambo magumu imezuia mambo mengi kutotokea, hasa mambo muhimu na magumu kwenye maisha yetu. Unafahamu kama kutofanya ulilopanga kufanya ili ufanikiwe ni kosa la kimkakati Unalolifanya sasa lakini majibu yake mabaya ni baaadae? au umeshasahau, maamuzi magumu ya wazazi ndio sababu leo uko hai? Acha uzembe nenda kafanye mambo makubwa na wala usiwe hata na chembe ya uwoga.

5. JIJIBU MASWALI UNAYOYAWEZA.

Yaelekea mwaka wa 2020 ulikuwa mgumu hasa pale ulipoambatana na gonjwa kubwa hili ya Corona #COVID na kiuhalisia umetupiga wengi, kiupana umepelekea baadhi ya sera kubadilishwa na hivyo kutufanya namna mpya.

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post