UKWELI WAKO, SIO LAZIMA IWE KWELI KWANGU.


UKWELI WAKO SIO UKWELI KWANGU.
Imeandikwa na 
GWEMELA CONRAD.
PHONE +255674167126.

Ukiona unakwama na ukatafuta ufafanuzi kutoka kwa mtu ambaye amewahi kupitia changamoto kama yako na akafanikiwa, baada ya kufanya kama yeye wewe usiweze kufanikiwa, hiyo inaweza kuwa na sababu au maana nyingi, 
 Mojawapo ikiwa ni kuwa tofauti na changamoto mnayofanana kuna vitu vingi viko tofauti kati yenu. Yaani kama kuna mambo aliyopitia peke yake ambayo wewe hujayapitia wewe, mfano ni yale ya kifamilia, kitabia na kiimani.
  SIKIA nikwambie kitu, HILI NENO MCHAKATO au PROCESS ndio kiungo Muhimu sana kwenye UKWELI WA YOOTE tunayo ASPIRE/TAMANI kuyapata... Yaani kama mtu atakushauri ufungue Duka na akakwambia utafanikiwa, Yawezekana ukafungua Duka na ukaishia kushindwa sababu zikiwa ni kukosa ukweli kuhusu mchakato(UFAFANUZI WA JINSI YA KUFANYA) wa kufanya unachotaka kufanya.
....UKIONA MTU 
1. anapalipwa ujue ni baada ya kazi hapo nyuma.
2. Ukiona mtu anapewa tuzo, inatokana mchakato wa kazi hapo nyuma.
3. Ukiona watu wanafurahia matunda, ujue kuna mtiririko wa mambo wamewahi kufanya ili wawe pale walipo.
4. Ukiona Mtu anafanya graduation ujue kulikuwa na hardtimes alizopitia.

So kwa yale mtu anayokuwa ameyapitia ndio yanakuwa UKWELI WAKE KWENYE MAISHA HALISI,kitu ambacho kinaweza kuwa uwongo kwako.
        JIFUNZE KUJIFUNZA UKWELI WAKO.
Wengi wamezoea kuangalizia walivyofanya wengine, mwisho wachache wanafanikiwa waliobaki wanafeli... KUNA UWEZEKANO WA WOTE KUFANIKIWA KABISA yaani kwa kujifunza changamoto zako, nini ufanye na wapi? unapaswa kuwepo kwa wakati gani? Au ni vipi uko tayari kukabili MSONGO na hata changamoto za kifedha..
Pia kutambua ukubwa wa Nguvu uliyonayo, na jinsi inavyoweza kuathiri kazi zako na miradi yako.
 Anza kujifunza, Endelea kadri unavyokumbana na changamoto zako kwenye yale unayoyafanya hata kama umeajiriwa...KITU KIMOJA KWA HAKIKA UTAKIJUA... YA KUWA MAFANIKIO YAKO YAMESHIKAMANA NA UTATUZI WA CHANGAMOTO YAKO BINAFSI NA KISHA CHANGAMOTO KWENYE JAMII YAKO..
👇
https://brightermango.blogspot.com/2020/12/michael-olunga-receives-japan-golden.html?m=1

''We believe, life is only a gift that expires and success in anything we have is not ours, its for human kind and so our wisdom'' -Gwemela

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post