JE? NI KWELI KWAMBA WANAUME WOTE WAONGO.

ULIMI MBILI..
Hivi umeshawahi kuwa na rafiki au ndugu ambae kila anachokiongea kinaonekana cha Maana lakini kwa kufuatilia kwako kidogo kidogo hujui kiliishia wapi kile alichokuambia? 
MTU MMOJA AKAIMBA HIVI
"HAWAMAANISHI WANACHOSEMA, LAKINI HUONGEA YA MAANA" Hawa watu tunawaita ULIMI MBILI kwa sababu moja tu, wao huwa wanasema mambo yatakayoendana na uelewa wako na vile ilivyo sahihi ili kupata Conset(ruhusa) yako.



Mfano mzuri ni mvulana anapojaribu kumpa matumaini makubwa msichana pale anapokuwa anamshawishi wawe kwenye mahusiano. Kutokana na rika au mtu, mvulana anaweza kumuahidi msichana Kuwa angemuoa, angemsaidia kwenye masomo yake,angetatua changamoto za nyumbani kwa msichana, Angemnunulia gari na vitu vizuri vingi vya kueleweka.
LAKINI NI KWELI ATATIMIZA HATA KIMOJA, TOFAUTI NA UPENDO ALIOJINADI NAO, MENGI KAMA HAKUWA NA UWEZO WA KUYATIMIZA MWANZO, BASI HATOWEZA.
Ukiangalia anachokuwa kasema mtu na mambo yanayofuata nyuma, hapa ndio utanielewa kwanini huongea ya maana, lakini hawamaanishi wanachosema.
.....Hata kwenye mambo ya Msingi wapo, mfano, wewe unatafuta kazi, lakini baadhi ya viongozi wa serikali wanasema kuwa kuna kazi na kiasi fulani wanajigamba kwa wananchi, kwenye uhalisia ukiingia huko mtaani, unakuta hakuna kazo yoyote.... nao pia tunawaita ulimi Mbili.


Au una rafiki, kila wakati unampelekea mapungufu yako, wakati wa wewe na yeye kuyatatua mapungufu yako, yeye anatoa udhuru, au hata iweje haumsikii akiongeza maboresho kama mwanzo, hii inamaanisha amechoshwa na anajutia ushauri wake... huyo nae ni ulimi mbili.
WEWE USIJALI,CHUKUA MAWAZO KAYAFANYIE KAZI...
TAKWIMU ZILIZO ANDALIWA NA GALLUP.COM ZINASEMA, "watu 10 kati ya 100 wanaotupenda, hukataa kuendelea kutupa msaada wanapohisi tu tutafaidika zaidi" Kwa hiyo ona ni jinsi gani Uko na watu wa aina ya ulimi mbili kiasi cha asilimia kumi ya jamii yako.

KUNA wakati unapaswa kua makini kwenye kupokea ushauri na pia kwenye kutoa ushauri, sifa ya ulimi mbili kubwa na nzuri ni "ATAKUELEKEZA VITU SAHIHI, LAKINI HATOKUSAIDIA AU VIKAMILISHA YEYE"

NAO PIA NI sehemu yetu, nao pia wana nafasi ya kurekebishika,tusiwapinge wala kuwanyanyapaa, Tusiwasute wala kuwapeleka kwenye mabaraza yasiyofaa.

IMEANDIKWA NA Gwemela Conrad Michael.
    Wa     +255626558019.
Email address gwemelaconrad@gmail.com
mailing address : box 53, kigoma.

Instagram @brightermango. 
Fb group Brightermango
Facebook Brighter Mango
Page Brightermango purpose

Thank you.
Photos by google.com

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post