JINSI YA KUONGEZA UFANISI WAKO KATIKA KAZI.

'JINSI YA KUONGEZA UFANISI WAKO.

Na brightermango.

 Unaweza kuongeza UFANISI wako wa kazi na ukaongeza THAMANI yako kwa kufanya mambo matano ya msingi.

Jambo la kwanza ni kuhakikisha kuwa UNAIPANGA siku yako na UNAKUWA NA VIPAUMBELE.

Kuna watu wengi sana wanapoteza muda na wanashindwa kupata MATOKEO makubwa kwa sababu kila siku yao haina mpangilio.

Kwanza, hakikisha hauanzi siku bila kuipangilia vizuri.



Hapa utatakiwa kuandika “To Do List” yako, yaani orodha ya vitu ambavyo kwa siku hiyo unataka kuvifanya.

Mbili, Ukishamaliza, unatumia orodha hiyo kuipanga kwa vipaumbele (Priorities), yaani unaanza kuchagua vitu ambavyo ni muhimu sana, muhimu wastani na vile ambavyo sio muhimu sana.

Tatu, unachotakiwa kufanya baada ya kuweka umuhimu ni kuhakikisha kuwa unaanza na kile ambacho ni cha muhimu zaidi bila kughairisha.

Usijiruhusu kuanza na kisicho cha muhimu wakati kuna ambacho ni cha muhimu sana haujakifanya.

Je, leo una orodha ya vitu unavyotaka kuvikamilisha?

Je, kitu gani muhimu zaidi unataka uanze nacho siku INAPOANZA?

#Gainwithgwemela
##gainwithbundi
#gainwiththeepluto #gainwithmchina #TimizaMalengoYako #Seeyouatthetop #joelnanauka #nanauka #mafanikio #ujasiriamali #biashara #miradi #STRAGEY2021

'We believe, life is only a gift that expires and success in anything we have is not ours, its for human kind and so our wisdom'' -Gwemela

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post