SHABIKI YANGA APANGA KUKIMBIA KIGOMA-DAR KWA MGUU ZAIDI YA 1000KM KUWASUPPORT YANGA.

 Mwanariadha Mang'suli Hussein (45) Mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji  ameanza safari ya kukimbia kwa miguu kutoka Kigoma Ujiji hadi Dar es salaam kwa ajili ya kushuhudia mechi ya Yanga vs Simba May mwaka huu ambapo anatarajia kutumia siku 18 kutoka kigoma hadi Dar es Salaam  kuanzia jana April 15.



Mwanariadha huyo amesema amewahi kukimbia kutoka Kigoma kwenda Kasulu (KM 95) kwa miaka mitano, na baadaye akakimbia kutoka Kigoma kwenda Tabora (zaidi ya KM 400 ) na sasa ni zamu ya Dar es salaam (zaidi ya KM 1200). 

Amesema lengo lake ni kwenda kushudia mchezo huo wa Watani wa Jadi lakini pia akilenga kuimarisha kipaji chake cha kukimbia na kuvunja rekodi ya kukimbia umbali wa KM zaidi ya 1000.

"Mimi ni shabiki mkubwa wa Yanga nimeamua kufanya hivi kwa moyo mmoja ili CV yangu ionekane mbali sana, nitatumia siku 18 kufika Dar es Salaam leo nitalala Kazuramimba, kisha alfajiri nitaendelea na kulala tabora naomba wadau wajitokeze wanisapoti kwa Jambo hili"---mang'suli Hussein.





'We believe, life is only a gift that expires and success in anything we have is not ours, its for human kind and so our wisdom'' -Gwemela

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post