KWANINI WATU HAWAISHI MILELE? NI RADHA YA MAISHA.?

RADHA YA MAISHA.
____________________
Na Gwemela.
----------------------

Ikiwa ni kawaida ya watoto wote kuuliza uliza maswali... Shabani, mjukuu wa mzee Shemsanga, alimuuliza swali mzee wake. SWALI LILIKUWA HIVI;

   SHABANI:👉NINI RADHA YA MAISHA IKIWA WATU WANAKUFA? KWANINI TU WATU WASINGE ISHI MILELE?.
--
Awali maswali yalionekana kana kwamba yalikuwa magumu sana... lakini mzee Shemsanga alikuwa tayari kwa kumjibu mjukuu wake swali lile.
--
BABU⤵
MAJIBU.
Maisha yana radha mjukuu wangu... na radha yake ni tamu na chungu.. ninajua utaniuliza kivipi? Majibu yangu ni haya.

KWANZA: Maisha yana tamu na chungu... au kupanda na kushuka..yana kuongezeka kwa thamani na kushuka kwa thamani ya vitu au mtu, ikiwa maisha yatakuwa juu tu siku zote, basi mjukuu wangu, pasingekuwepo na watu kuota/kutaka kufanya vizuri zaidi, labda pengine kusingekuwepo na matumizi yoyote ya akili au hata matumizi ya mawazo yenye ishindani...labda usingewajua wanasiasa na wanaharakati kama Mange Kimambi , Malisa GJ , Veronica France  na KIGOGO 2014 & MDUDE  na pengine usingeijua elimu yoyote  iwe uchumi,siasa sayansi au hata elimu ya deen... lakini pia pasingekuwepo na jitihada au utatuzi wa changamoto hapa Duniani.
       Hebu fikiria hili.... kama matajiri wa sasa wasinge ogopa kushuka kiuchumi basi wangekuwa wamelala tu na hata jogoo angepo wika wao wangeamka wakiwa kwenye meli kubwa za starehe... lakini wala.. wao huwa makini kila siku kutatua changamoto za watu... na wengine huita kile wanachokifanya ya kuwa ni "Passion" yaani jukumu lao kimaisha, inafikirisha pia kuamini kuwa, asilimia kubwa ya uhai wa mtu unakuwa kwenye matumizi mazuri pale anapokuwa anafikiri katika kupambana na changamoto. Na ama kwa hakika hicho ndicho kinachofanya maisha yawe na radha... na mojawapo ya radha hiyo ni KUPANDA NA KISHUKA KWA MAMBO.
kama ilivyo kwenye utambuzi wa mgonjwa kwa kupitia mapigo ya moyo hospitalini, ya kwamba yakiwa yako sawa tu..na  msitari wa mapigo ya moyo umenyooka...basi madaktari watatafsiri kuwa mgonjwa wao amefariki... na ndivyo pia ilivyo kwenye maisha... kama mambo yatakuwa hayana panda shuka... basi tambua mwisho wa maisha umekaribia.  Mwisho wa maisha unaweza kukaribishwa kwa kukata tamaa, NDIO KUKATA TAMAA SHABANI, mtu akikata tamaa... huwa anamaanisha hayuko tayari kukabiliana na panda shuka za maisha, inaweza pelekea yeye kujiua aidha kwa sumu au hata kujinyonga... kitu ambacho si kizuri hata mara moja.

PILI; kutokutabirika kwa matukio yajayo mjukuu wangu... hii nayo ni radha ya maisha. Na ikiwa hujaielewa... ngoja nikupe mifano miwili, mmoja wa furaha  na mwingine wa hudhuni...
Ukiwa unatembelea kumbi za kuonyesha mchezo mpira na ukakuta watu wakionyesha mchezo wa mpira uliokwisha kuonyeshwa awali(uliopita), wewe mjukuu wangu, utakuwa radhi kulipia mchezo huo?, la hasha, hutolipia kwa sababu mchezo ule tayari ulishapata majibu yake wakati uliopita.. ila utalipia tu kama mchezo wa mpira ule utakuwa ndio mara ya kwanza kufanyika na kurushwa moja kwa moja.
Au ikiwa uko nyumbani,shuleni na unapewa taarifa za msiba, binafsi tukio kama hilo unakuwa hukulitegemea ingawa lipo kila siku au hata aloyekuwa anaumwa alijieleza kuwa angefariki muda wowote, hili linafanya radha ya maisha iwe chungu kwa walio wengi na pia inafanya pia radha iwe tamu kwa wachache mjukuu wangu(wasiompenda marehemu).
--
SHABANI: Babu vipi kuhusu maskini?
--
BABU: Hakuna mtu anayeitwa maskini akiwa hai mjukuu wangu; ila nitakujibu; Radha nzuri ya maisha ni furaha..  na furaha haiko kwenye kiasi cha juu au thamani ya juu ya vitu ulivyonavyo.. ila iko kwenye kuridhika na vile vingi au vichache ulivyo navyo.

Hebu fikiria hili mjukuu wangu,  vipi kama kila linalokuja tungelijua, unafikiri kuna mtu angemuheshimu mtu mwingine..au kuna wakati watu wangemshukuru muumba wao? Ama kwa hakika woote wangeacha kuwa na mioyo ya shukrani..kitu ambacho ni hatari zaidi ikiwa kingetokea. Japo radha kuu za maisha ni mbili, yaani chungu na tamu... inafikirisha sana kuamini kwazo yakwamba zinampata kila mmoja hapa DUNIANI...na jawabu lake ni kuwa mwenye shukrani siku zote za maisha yako huku ukipambana kuzishinda changamoto.
--
SHABANI: sasa Babu nini kinaweza kufanya tubaki au turudishe kwenye uhalisia baadhi ya matukio kama sherehe na misiba???
--
BABU: Kitu kinachofanya radha za maisha zilizowahi kututokea tuwe nazo hata tukiwa wazee mjukuu wangu ni Kumbukumbu... wengine hawatamani kukumbuka baadhi ya mambo kwenye historia yao ya maisha....lakini pia kuna wengine wanatamani kuyakumbuka maisha yao ya nyuma nyenye furaha... hii ikiwa tu walipo sasa hivi wanahudhunika au kukasirishwa na ugumu wa maisha. JE?hata sasa si kuna wengi tu hawataki kuishi kwenye uhalisia wa sasa kwa sababu tu wataonekana ni maskini..au wengine hawako hivyo (yaani hawatamani maisha haya yabadilike)

Mwisho wa DAYALOJIA HII(DIALOGUE).
--------------------------------------------------------------------------------------

SOMO: MAISHA YANA RADHA MBILI...CHUNGU NA TAMU, ZOTE HUWAPATA WOTE WASIOKUWA NACHO NA WALIO NACHO...JARIBU KUISHI NDANI YA RADHA ZOTE MBILI.

_________________________________________________________
Call +255674167126
Whatsapp tu.

Fuata/follow page yetu ya Brightermango purpose
Fuata/follow account yangu ya fb Brighter Mango
Au jiunge na group langu la Brightermango

Gusa hayo maandishi yenye weusi wa kuiva ili unifollow.
-----------------------------------------------------------------------------------------


''We believe, life is only a gift that expires and success in anything we have is not ours, its for human kind and so our wisdom'' -Gwemela

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post