NGUVU YA KUTAMANI/SIRI YA UTAJIRI INAYOTUMIWA VIBAYA.
Leo nakutafunia baadhi ya mawazo ya Bwana mmoja aitwaye Napoleon Hill aliyeandika vitabu vingi vya kuhamasisha matumizi ya fikra ili kufikia maendelea binafsi ya kiuchumi.
****
Ukiwa unafanya jambo kwa juu juu... matokeo yake pia yatakuwa ya juu juu, na ukifanya kwa kuzama basi matokeo yake pia huwa makubwa na yenye kufurahisha.
****
Mnamo miaka ya 1900s au mwanzoni mwa karne ya ishirini, palipata kutokea mwandishi mashuhuri, mtu aliyetengeneza utajiri wa watu kwa kutumia wino wa karamu yake, aliyetumia falsafa yake kumfanya mwanae aliyezaliwa na kuaminika kuwa asingeweza kusema na kusikia, akaweza kusema na kusikia. Mwandishi ambaye matajiri wakubwa wa muda wote wa Marekani kama D Rockerfella, na hata wagunduzi au wavumbuzi wakubwa kama Thomas Edison alva, pamoja na wajasiriamali waliofanikiwa hata leo kama Henry Ford(mmiliki na mwanzilishi wa magari ya Ford nchini Marekani) wanaamini na kukiri kufanikisha hayo yote kupitia falsafa ya napoleon Hili... Falsafa ya TAMAA.
......
Tamaa inayozungumzwa hapa sio ile ya kudhulumu, itakayozungumzwa hapa sio ile inayokera na kufanya hata baadhi ya watu kuuwawa kwa sababu wametamani vitu wasivyonavyo ba kuona kuiba ndio njia mbadala.
Tamaa ya maendeleo binafsi ndiyo itakayozungumzwa hapa.
$$$$
Kutoka kwenye kitabu chake cha "THINK AND GROW RICH"
ANAADIKA HIVI.
Tamaa ya maendeleo inatengenezwa na kila mtu anaweza kuipata, kila kitu kilichopo kwenye mfumo wa akili au uelewa ndio hufanyiwa kazi, hivyo ikiwa utakuwa na tamaa halisi yaani "DESIRE" na Sio haja yaani "WISH" basi yote unayoyatamani yatatokea.
Ikiwa kama tunataka kubadili historia au desturi ya maisha yetu... haina budi kwenda kinyume na mama DUNIA kwani mama huyu ametuaminisha ya kuwa hapa tulipofika ndio penyewe na hakuna zaid ya hapa. akitolea mfano wa wakati ule, Hill anasema, ugunduzi wa radio ulionekana kama kituko ... lakini ndani yake kuna ushahidi wa wazi wa mtu asiyekata tamaa kubadilisha jinsi Dunia inavyoyachukulia mambo... wakati ugunduzi wa radio ukifanyika... nchini Marekani na kwingineko walikuwa wakitumia waya kusafirisha sauti na hii ilijenga hoja ya kuwa hakuna mtu abgeweza kutengeneza mfumo au teknolojia ya kusafirisha sauti pasipo na waya.. au kwa kutumia anga. Lakini Bwana Cork licha ya kuonwa au kutazamwa kama kichaa na rafiki au hata ndugu zake, yeye alijaribu kutengeneza teknolojia hii...
Napolen anaendelea kwa kusema, ikiwa Cork hakujua kilichokuwa kinampa ujasiri, basi mimi nitawaambia... Kilichompa ujasiri cork ni ile Tamaa ya kutaka kilichomo kwenye fikra yake au kwenye taswira ya uelewa wake kionekane kwa watu.. tamaa ya kutotaka kushindwa, tamaa ya kutaka kudhirisha kwa wanadamu kuwa hakuna linaloshindikana. CORK ALIFSNIKIWA KUTENGENEZA RADIO YA KWANZA... raisi wa awamu hiyo alipongeza na kusema... badala ya kuzunguka Nchi nzima kufikisha ujumbe mmoja...sasa nitatumia radio kuwafikia mamilioni ya watu na itaharakisha maendeleo yetu binafsi na ya nchi yetu ya Marekani.
president kenyatta... railway #madaraka day. |
🐮✏📖
Hatua za kufanya ili ulitunze na kulifanya wazo lako liwe hai hadi kufikia ndoto zako.
1. Chambua mawazo yako yote na uangalie ni kipi ungetamani kurekebisha, boresha au hata kubadilisha... haijalishi ni kwenye siasa elimu au sayansi...kitu chochote.
2. Tambua watu wanaoweza kukuboreshea mawazo yako yakawa na uhai kila siku ili kukumbusha azma yako.. hapa watu wa kukumbusha ndoto yako huku wakiwa na shauku ya kutaka kuona maendeleo yako.
3. Iambie akili yako kuhusu ndoto yako hii ... huku ukiiaminisha kuwa kile unachoenda kukifanya kinawezekana.
4. Amini na jiamini kwenye upande wako wa ubunifu. Watu wanaweza wasiamini sana unayoyaona ndani ya mawazi au ndoto zako... hii ni iwa sababu wewe ndio uliyebeba hiyo ndoto... ikiwa kama uatafanya na watu wakawa wakishuhudia basi kuna uwezekano kabisa ukawabadirisha mitazamo yao.
5. Ukianza kuiona ndoto yako... unapaswa ujue kuwa hakuna kitu kikubwa Zaidi ya kuiboresha.. maana mahitaji yanabadilika na Dunia pia inabadilika... hii ni kwa sababu ya muingiliano wa watu na vitu.
6. Rudisha uelewa wako kwa jamii.. wafundishe rafiki ndugu au watu wako wa karibu ili ukiondoka mawazo yako yaishi.. au ukiweza andika kitabu kitakachofungua fikra za watu kukuhusu au kuyahusu yale uliyoacha na jinsi ya kuyaboresha au kufaidika nayo.
KUMBUKA HILI.... KILA SIKU IAMBIE AKILI YAKO INAWEZA KULITIMIZA LILE ULILOFANYA .... LILE UNALOTAKIWA KUREKEBISHA, LILE UNALOTAKIWA KULIONDOA KWENYE SIASA AU KULIBIRESHA.
silaha kubwa ya mafanikio ni uelewa wa mtu.. uelewa wa kuamini hakuba kinachoshindikana, ni uelewa muhimu sana ni uelewa wenye kujenga, ni uelewa wenye kukufanya uboreshe kila siku sehemu ndogo uliopo hadi pale itakapokuwa kubwa.
CHAGUA CHANGAMOTO... IFUNGUE/ITATUE/IONE JINSI YA KUIFANYA IWE SULUHU BDANI YAKO... UKIMALIZA KUITATUA MOYONI *TAMANI* SASA KUITATUA KWENYE MAISHAA YA KWELI...
UKIFANYA HIVI , ITAKUWA RAHISI KUFIKA WALIPOSHINDWA KUFIKA WENGINE.
Imeandikwa na Gwemela Conrad Michael.