UNAFAHAMU NI KITAMBOO....
Tangu umuombe msamaha Mungu, tena ni muda sasa hujasema asante Mungu kwa uhai, hujasema asante kwa afya, wala hujasema asante kwa neema ya kazi na chakula, yaani kifupi ni kitambo sana sasa, umekaa bila kumtambua MUNGU kuwa ni muweza wa yote kama ulivyokuwa kwanza.
ulikuwa Duni wewe, yeye hakukutweza bali aliteta na watesi wako, na akakupatia hitaji lako la moyo, ulikuwa fukara wa kutupa wewe, sasa amekuvika hariri na silk. yeye hahitaji chochote kutoka kwako, maana hata dua zako za zamani ulizompelekea hakuwa na uhitaji nazo, maana kama ni kuabudiwa, anao maelfu na malaki na mabilioni ya Malaika wamwabudio kwa haki, yeye hakukupenda kwa sababu wewe ni mwema sana, au labda una mtumikia sana, la, yeye alikupenda na atazidi zaidi kwa sababu ya lile agano lake la kwanza kwa watu wote... AGANO LILE LENYE MANUNUZI YA THAMANI, AGANO LILE LA UKOMBOZI, ambalo alilitangaza kupitia matukio mbalimbali, kwanza kupitia Ibrahimu kwa kumuamuru Yeye Ibrahimu amtoe sadaka mwana pekee, hili liko KWENYE Kitabu cha MWANZO 22:1 -15.
yeye aliahidi kuwa atatukomboa pale ADAMU Alipomkosea MUNGU, na kujenga msingi wa agano lake...kwakua MUNGU NI MWAMINIFU, Basi sasa yale aliyoyapanga huwa...na kila anachokifanya ni kwa sababu ya upendo MKUBWA alionao kwetu, yeye hajawahi kujitenga na wale woote wanaomlilia na wasio mlilia.
IKIWA UNA HISI HATIA MOYONI MWAKO, na kujisemea, nitatubu na kumwambia MUNGU ANIPE MSAMAHA, hilo ni sawa sana, na ikiwa utataka kufanya hivyo basi usichelewe, maana MUNGU anautambua msamaha wa yeyote yule na hata kama ni mauaji, Hebu angalia hapa Kitabu cha kutoka 2:12 " Basi akatazama huko na huko na alipoona ya kuwa hapana mtu, akampiga mmisri yule , akamaficha ndani ya mchanga." na kwa sababu Musa alifanya kwa hila basi yaelekea angepaswa kulipa kwa damu maana huku nyuma kwenye kitabu cha mwanzo 4: 10, Kaini alipewa adhabu kali kwa kumuua nduguye habili na sauti ya Damu ya habili ilimlilia Mungu...
MUNGU ANAWEZA YOTE NA ANATAMANI UYARUDIE MAISHA YAKO YA KWANZA.
alikuwa rafiki kwako, rafiki na si kama wanadamu, alikuwa Mungu kwako, na si kama miungu ya wanadamu, alikuwa baba kwako, lakini si kama mababa wa Dunia hii.
amekupitisha shule ili akupe picha ya nini kinaendelea kwa wanadamu wenzako.
amekutenga na watu wabaya, lakini wewe umesema hawa ndio ninaowataka mimi, amekufungia ndani na kukuimbia nyimbo nzuri za gitaa na vinubi kwa ushairi wa mashairi ya DAUDI lakini umesema hapana na kukamilisha vile alivyosema Suleimani, MHUBIRI 10:2 " Moyo wake mwenye hekima uko upande wa kuume; bali moyo wake mpumbavu uko upande wa kushoto." maana wenye hekima husema
"HERI KUSIKIA LAUMU YA WENYE HAKI,KULIKO MTU KUSIKIA WIMBO WA WAPUMBAVU" muhubiri 7:5.
Nawe umezidi sana kuisikia sauti ya adui hata ukaiacha njia ile nzuri ya UKOMBOZI, njia ambayo kuipita ni rahisi kwa sababu ya kifo chake Yesu kristo.
DAMU NA SADAKA SAFI YA KUTEKETEZWA KUTOKA KWA YESU KRISTO MASIHI WAKE NA MPAKWA MAFUTA WA KITI CHA ENZI, MUNGU ALIYETOKA KWA MUNGU, MUNGU KWELI KWA MUNGU KWELI, NA MUNGU MUUMBA WA VYOOTE.
Maana neno nini sasa, ikiwa twaona aibu kulifundisha, basi si kitu tena, kwani hata yaliyomo ndani yatasadikishwa na wapotofu kuwa ni upotoe UTOKAO KWA mtu kWENDA Kwa watu, na OLE WANGU MIMI NISIPO IHUBIRI INJILI.
FADHILI ZA BWANA MUNGU ZIBAKI KWENU NYOOTE!
BARUA YA UJUMBE SAFI KWA WOTE
IMEANDIKWA NA MINISTER GWEMELA CONRAD MICHAEL
Under Brightermango Purpose charter.
"Butterflying ideas to you. We make your day, brightens it and inspire your night"~GWEMELA