KIGOMA MASHUJAA FC VS PAMBA FC. HAKUNA KIINGILIO.

Siku ya leo tupo tayari kufia uwanjani wala hatutakuwa na mizaha, tuna njia mbili tu, ima tufie uwanjani au tuingie ligi kuu basi, 



Ni siku ya leo Jumapili tarehe 21 Saa 10:00 jioni ndani ya Lake Tanganyika Stadium, Mashujaa FC Watakabiliana na Pamba FC kutokea mkoani Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Mh Thobius Andengenye amewaka dau la Tsh 200,000/= kwa kila goli 1, Mh Salum Kali DC-KGM goli 1 dau lake Tsh 100,000, Eng. Maftah goli 1 sh 100,000, Maj. TIKA (Com CHUI) sh 100,000 kwa kila goli 1, na Ndg Baruan MUHUZA goli 1 sh 50,000.

Hamasa Inaanzia Kwa Mashabiki Kuhakikisha Mnakuja Kwa Wingi Kuujaza Uwanja, Popote ulipo hii ikufikie Tarehe 21 unapaswa kufika Katika Uwanja wa Lake Tanganyika Kuipa Hamasa Timu Yako pendwa.

Hakutakuwa na kiingilio MECHI NI BURE na milango itakuwa wazi kuanzia majira ya saa 8 mchana.

Siku ya Jumapili itakuwa ni vita dhidi ya.
Ubora wa Ziwa Tanganyika vs Ziwa Victoria.
Ubora wa mafuta ya Mawese na Mafuta ya PAMBA.
Ubora wa Mgebuka na Sato
Ubora wa Kuhe na Sangara 

WanaKigoma tunaomba mje kwa wingi Pamba FC Watapigwa kama ngoma za mizuka.

Tukiungana Kwa Pamoja Tunaweza, Lazima Tushinde Michezo yetu yote ya Playoffs

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post