JINSI FURSA HIZI TANO ZA DHAHABU ZINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KIJANA WA KIZAZI HIKI 2020.

JINSI FURSA HIZI TANO ZA DHAHABU ZINAVYOWEZA KUKUSAIDIA,

KWANI HAPA TUMEFIKAJE?

Unapoamua kuianza safari yoyote lazima kuwe na uelekeo wa safari husika. na kama unapelekwa na mtu basi mtu husika ndiye anayeweza haswa kukuambia uelekeo wenu wa safari. safari inahusisha mfululizo wa matukio mengi sana kiasi cha kutopata wakati au nafasi ya kuuliza uelekeo husika.

Turudi kwetu sisi vijana, kwani tuko wapi hapa, na je hapa tulifika vipi? au tunajua nini kuhusu mahali tulipo kwenye ulimwengu wa ubunifu sayansi na teknolojia.? kwa maoni binafsi ni kwamba, ninaweza kujua niko wapi kwa kuyachunguza mambo yafuatayo,:-

1. Uwepo au upatikanaji wa fursa.

Kwa jamii ya sasa ambapo mimi pia niko kati yao, fursa za maendeleo ni kubwa sana na zimepanuka kwa kiwango cha juu. Ingawa fursa ni nyingi ila haziko wazi kihivyo kwa vijana wote, kwa maana fursa zenyewe zinawataka vijana wawe na ujuzi au maarifa fulani ili kuweza kuzikabili au kuzichukua. kwa mfano, ili kijana aweze kuitumia kwa faida mitandao ya kijamii na kuweza kujiingizia kipato inampasa awe ana ujuzi wa matumizi yake(hiyo mitandao ya kijamii) na pia awe anaweza kuwasilisha mambo muhimu na hitajika kwa jamii pia lazima awe na uvumilivu wa kutosha… kiasi cha kuvumulia kushindwa kufanya vizuri hadi hapo atakapoweza kufanya vizuri.  hivyo hii hali au haya mazingira yanaonyesha kabisa tulipofikia au tulipo vijana ni KWENYE KIZAZI JANJA.

2. Ukomavu wa tehama na teknolojia.

Wakati huu wa sasa, mambo mengi yenye uhitaji wa matumizi ya usaidizi wa teknolojia yanaibuka kwa kasi kama, mtu akitaka kuchora au ku sahihisha picha, anaweza kutafuta programu ya simu au tarakirishi kwaajili ya usaidizi huo, mfano wa programu hizo ni ile ya google  ijulikanayo kama “nano banana” au ile ya “microsoft-pilot” na hizo ni kwa uchache tu. pia mtu aweza andaa programu ya kompyuta kwa kutumia teknolojia na kisha kuamuru ifanye kazi kadiri ya mawazo yake ili kufanikisha anayoyawaza au kusudia. Hii ni ishara ya wazi kuwa kwa sasa tuko kwenye ulimwengu wenye ukomavu wa tehama na teknolojia iko kati hatua ya juu na kubwa kulinganisha na hapo awali.

3.  Upatikanaji wa taarifa(data set) kamili.

Hii kwa sasa inawapata wakaazi wote wa dunia, nikiwa na maana kwamba, ikiwa wewe ni mtumiaji wa tarakirishi au simu jana, wewe pia unanufaika na upatikanaji wa uhakika wa taarifa pasipo na shaka tena kwa wakati, na hili linamaanisha kwamba tuko kwenye ulimwengu wa kidijitali. yaani zamani wengine wangetumia muda mwingi kujifunza kupitia vifaa vya kidijiti lakini wasingefanikiwa kwa haraka kwani kwa wakati wao hawakuwa na vifaa vyovyote vya kidijiti bali vile vya analojia ambavyo vilihusisha mwonekano hafifu wa taarifa na pia vilihusisha ucheleweshwaji wa taarifa. kwa Ushahidi huu nikuwa sisi ni wenye bahati na tuko kwenye wakati mzuri zaidi, tuna fursa pana ya kufikia ndoto na malengo yetu.

4. Upatikanaji wa vifaa vya usafirishaji.

Uwepo wa vifaa saidizi vya safari vyenye mwendo-kasi na upatikanaji wa “self-powered” motor kwa njia ya umeme vimeboreshwa kwa kiasi kikubwa, ambapo mtu anaweza kukamilisha mahitaji ya kawaida ya usafirishaji kwa wakati na kwa umakini mkubwa kulingana na uhitaji wake wa nafasi ya muda au matokeo anayotamani yawe. yaani kuliweka hili katika mtazamo ni kuwa mtu anaweza ondoka amekunywa chai Tanzania na kula chakula cha mchana nchini China. hii inawezekana kwa matumizi ya ndege au “rockets” ili kufika haraka mahali kwa mahali.
Huu ni ushahidi wa moja kwa moja kwamba Dunia au ulimwengu uko karibu zaidi kuliko hapo zamani na nyakati zozote zile zilizowahi kupita.

5. Maarifa ni kama bure.

Dunia hii na wakati huu, ukijibidiiisha unajua mambo unayotamani kuyajua lwa urahisi haswa kwa kuungamanisha matumizi ya ushahidi a, b, c, d uliotangulia hapo awali, kwa teknolojia unaweza fungua kurasa mtandao zenye mafunzo ya unuzi unaotaka wewe kujifunza, au unaweza fikia haraka taarifa kwa kutumia vifaa hivyo vya kidijiti ambavyo vimeungaishwa na mtandao ili kukuwezesha kuzifikia taarifa za maarifa husika, pia unaweza kuwa unajifunza au kusomea mbali na kurudi sehemu nyingine kwa kutegemea usafiri, mfano Mohammed Dewji alisomea nchini Marekani na sasa anaishi Tanzania, safari zake nyingi kama si zote inaelekea alizifanya kwa kutegemea usafiri wa ndege.
Huu ushahidi ni kwamba sisi tunaishi wakati wenye manufaa na nasafi za kutosha kufikia malengo yetu binafsi.

Ziada! uwepo wa teknolojia ya mtandao(internet) inaweza kuwa ndio kiungo muhimu zaidi ya vyote nilivyotaja hapo juu ili kufanikiwa kusonga au kusogea mbele zaidi.
siku hazigandi anza kuzikaribia fursa hizi kubwa ili kusogea mbele zaidi na kuyajongelea mafanikio yako.




Imeandaliwa na kuletwa kwako na,

Gwemela Conrad Michael, CEO
 brightermango.

2025, 09, 17.


"Butterflying ideas to you. We make your day, brightens it and inspire your night"~GWEMELA




Katonga.

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post