FAST AND MOBILE EDUCATION
(F.M.E) FOR BODABODA AND SPECIAL GROUPS AT KISARAWE.
BY Gwemela Michael.
Blogger.
UTANGULIZI.
Kutokana na takwimu zilizopo za wizara ya afya zilizotolewa
na vyombo vya habari zinaonyesha kuwa kuna uwepo mkubwa wa vifo wa vijana wenye
umri kati ya miaka 15-29 kwa njia ya ajali, ikifuatiwa na kujiua Kutokana na
changamoto mbalimbali za maisha.
·
Kwa
uwepo wa vifo hivyo, sisi afrotalent, vijana ambao tupo kwenye rika hilo
tumeamua kuingilia kati na kupunguza kama ikiwezekana kuzuia vifo hivyo.
·
Kwa
kuanza na wilaya ya kisarawe, tunatamani kufanya yaliyo orodheshwa hapo chini.
JINA LA MRADI: FAST AND MOBILE EDUCATION
(F.M.E)
F.M.E, ni
mradi mahsusi Kwa makundi maalumu kama yatima na wasiojiweza, pia unawahusu
watu wote wanaokosa elimu ya msingi kuhusiana na changamoto zao za kila siku,
kama vile bodaboda na vibarua.
Huu mradi ki
ufupi unawahusu watu wote wenye uhitaji wa elimu ya kiuchumi na kijasiliamalia
haswa kutoka kwenye hali dhaifu na mbaya waliomo, na kujikwamua kiuchumi.
ENEO.
Wilaya ya Kisarawe.
MISINGI ELEKEZI.
A. KUJIDHATITI.
Kujitoa kwa dhati kwenye mradi huu pasipo na wasiwasi na kuhamasisha kwa
uelewa wetu wote.
B. HESHIMA.
Kuheshimu kila program ambayo tutaiweka katika vitendo kwa kuhakikisha
uwepo wa uhalisia wa program husika.
C. HUDUMA YETU.
Kusimamia na kutekeleza mradi huu wa (FAST
AND MOBILE EDUCATION) Kwa Makundi
maalumu pamoja na makundi yasiyo maalumu ila yako kwenye hatari ya kudhurika na
mazingira kama bodaboda.
WAHUSIKA.
SPECIAL GROUPS.
copied: from ctc-ck.com ctc-ck.com
2. Mobile na fast education kisarawe
itawahusu watoto wote wanaoishi kwenye mazingira magumu na pia Makundi mengine
yote special kama wakina mama wajane, vilema,vipofu,ulemavu wa ngozi(albino).
3. WATU MASHUHURI NA MAARUFU.
Watu maarufu kama Mh.
Mkuu wa wilaya, Jokate Mwegelo na watu wengine wote walio maarufu kama
inspiration icon kwenye maisha yetu ya kila siku pasipo na uwepo wao, yamkini
elimu kwa ushuhuda itakosekana na pia itapendeza kama watu hao mashuhuri
watatoa ushuhuda unaoendana moja kwa moja na maisha magumu wanayoyapitia watu
hawa.
4. SERIKALI.
Wahusika wa ngazi hii ni
serikali kwa ujumla ambapo kwa mradi huu umerengwa moja kwa moja kwenye ngazi
ya wilaya ya kisarawe, hivyo uwepo wa shughuli hii katika ngazi ya wilaya,pia
shughuli hii itafanyika katika ngazi ya wilaya.
Na hawa ndio watakaokuwa
wamiliki wa mradi huu Kutokana na uhalisia wa mradi wenyewe, yaani utafanyika
ndani ya wilaya ya kisarawe na pili utawahusu viongozi wa kisarawe na mwisho
utapewa nguvu na halmashauri/manispaa ya kisarawe ili kuleta madhara chanya.
5. AFROTALENT.
Hawa ni wanafunzi wa chuo
kikuu cha Dodoma ambao wanabeba ndoto zilizokufa za jamii nyingine ikiwemo ile
ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu huku wakikosa elimu,chakula,mavazi
na hata pa kulala na hivyo kujikuta wakilala maeneo hatarishi kama kwenye
misingi ya madaraja na wakati mwingine kufariki kwa kupitiwa na mvua, pia hawa
vijana hutoa elimu ya ujasilia mali ambapo wanasema kuwa ‘‘Elimu ya shuleni kwa mtu aliyekwisha ikosa
sio dhambi kwake kiasi cha kujilaumu
milele bali anaweza kujifunza elimu msingi na kujua yeye ni nani na kisha
kukuza talanta yake hiyo njema’’.
Afrotalent inaundwa na
MICHAEL NKANWA na GWEMELA CONRAD MICHAEL ikiwa na member takribani 40 ambao
wamekuwa kama volunteer katika shughuli mbalimbali za afrotalent na hivyo
kupeleka Mbele baadhi ya shughulina kufanya zifike kwa kiwango kile ambacho
Tulikuwa tumekusudia.
6. WANACNCHI.
Wananchi wa kisarawe wote ni
walengwa wa mradi huu kwa unalenga
kuingia kwenye jamii yao moja kwa moja ili iweze kuwa na fursa ya kuwapatia
Makundi maalumu ya watu ili kuwafungua na kuwajengea hatima yao kwa
kuwashawishi washiriki kwenye baadhi ya programu ambazo zitakazokuwa zikifanyika
UTEKELEZAJI
WA MRADI.
Mradi na
utekelezwaji wake utakuwa kwenye programu mbalimbali katika jamii ya Kisarawe
kama ifuatavyo;
PROGRAMU.
Mobile na fast EDU ndani ya kisarawe itakuwa na majikumu ya
kuendesha programu mbalimbali ili kuhakikisha adhma yake ya kuwafungua Makundi
maalumu ya wasiojiweza ili kufanikisha malengo yao ya kila siku ili Kujenga
jamii imara ambapo kila mmoja wetu anaifurahia. Zifuatazo ni programu
mbalimbali ambazo zitafanyika kwa wakati mradi huu.
1. MOBILE AND FAST EDU.
Itakuwa ni programu yetu
ya kwanza ambapo ina lengo ya kuwafikia walengwa takribani 10000. Programu hii
ina lengo la kuwafikia watu wote walioko kwenye mkusanyiko wa Kundi maalumu
ambao hawakupata elimu ya kusoma na kuhesabu.
Kwa kutumia mfumo wetu wa
“I teach you and you teach me” programu itawafikia wahusika tajwa kwa haraka na
kuwezesha watu husika kuelewa kusoma na kufanya hesabu ndogo ndogo ambapo
itawasaidia kwenye kujijenga kiuchumi.
-
Kwa
kipengele hiki cha mobile and fast edu, watoaji wa elimu watakuwa ni
a) Traffics, hapa mkuu wa matraffic
atazungumzia usalama na sheria za barabarani
b) Viongozi wakubwa wa serikali, watatoa
mwongozo wa kisheria wa wapi watu hawa wanapaswa kufuatilia haki zao za
kimsingi kisheria ili kuwezesha ndoto zao.
c) Wanafunzi wote waliokwishafanikiwa
ambao asili yao ni wilayani kisarawe watapata nafasi ya kuongea ili waweze kuja
nyumbani kufanya motivational talks na kuwa hamasisha watoto,vijana,wakina
mama,na wazee na wale wote waliokata tamaa ya maisha
d) Mwisho kwenye program hii ni
afrotalent ambao hawa watatoa elimu juu ya namna ya kuishi katika mazingira
magumu na kutoa elimu ya ujasiliamali ili kuepuka ajali za barabarani na
Kujenga ajira nje ya bodaboda.
2. SAFE BIKE FOR SAFE KISARAWE.
picha:copied from mwananchi.co.tz
-
Hii
itakuwa program ya pili ambapo kila kijana atashiriki haswa kwa vijana
wanaoshiriki uendeshaji wa bodaboda na hivyo kutoa impact kwa jamii husika ya waendesha
bodaboda ili kuwezesha usafiri wa bodaboda ni salama na pia kuminiwa na wateja
wake.
-
Takwimu
u zinaoenesha vifo vingi vya vijana vinatokana na ajali, na chanzo cha pili cha
vifo hivyo ni kujiua . Ambapo kwa upande wa ajali ni ajali nyingi zinazohusishwa
moja kwa moja na zile za vyombo vya moto hasa barabarani.
-
Hivyo
kwenye program hii tutatoa elimu kuhusu namna nzuri ya kutumia vyombo vya moto
kabla,wakati na baada ya kuendesha bodaboda kwa kuwatembelea kwenye vituo vyao vya
kazi.
-
Mfano,
kama pikipiki imewekewa mafuta na dereva anahisi mafuta yamekwisha, sisi
tutampa funzo hili… FUNZO; mafuta hasa ya petrol yanaweza kulevya hivyo kwa
yeyote anaeendelea kunusa kama ishara ya kujua ujazo wa mafuta hapo huwa
anakosea kwani anachokifanya ni kuvuta kilevi pasipo kujua na hivyo kushambulia
mfumo wake kati wa kufikiri na hivyo kumfanya awe maamuzi hafifu hivyo hata
kwenye eneo la barabarani anaweza kutafsiri alama ya kutopita kwenye njia ya
wapitamiguu kama ni eneo lake. ….NINI TUFANYE? Sisi kama bodaboda tunapaswa
kujifunza kujua mafuta yakiwa yamekwisha kwa kuangalia kwenye dashboard.
-
Mfano
wa pili ni uwezekano wa pikipiki au gari kulipuka wakati wa kujaza mafuta huku
vyombo hivyo vikiwa vimewashwa. Hivyo jinsi ya kufanya ni kuzima gari au
pikipiki na hivyo kuzuia ajali.
3. MY SCHOOL MY CARRIER.
copied from: amazon.co.uk
Kwenye program hii hapa
kisarawe itafanyika kwenye shule zote za secondary na zile za msingi ili
kuhamasisha ufaulu wa darasani huku ikiwa na lengo kuwafanya wanafunzi wenyewe
kuwa na uwezo binafsi wa kujiendeleza hata kama watashindwa kujifunza na elimu
ya juu ya upili kiasi kwamba wataweza kujijenga kiuchumi na kuachana na mawazo
ya kushiriki katika udereva wa bodaboda na kuhakikisha wanakuwa na uelewa wa
moja kwa moja kuhusiana na madhara ya barabara.
-
mambo
yatakayofanyika moja kwa moja ni kutoa jtatu jioni moja na jmosi moja kwa ajili
ya elimu kwa vitendo kwa kila wiki na hivyo kuwapa fursa vijana wa kidato cha
tatu na kidato cha nne kuhudhuria ili
waweze kukutana na elimu hiyo muhimu ili iwe msaada kwao hapo baadae.
-
Kwa
upande wa wanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani yao watatakiwa wa adopt hii
program ya “I read, you read, we read”. Ambapo kwenye program hii kila darasa
litasimamiwa na mwalimu wa darasa na huku wanafunzi watahusika na eneo lingine
lote la programu hii litafanywa na wanafunzi wenyewe.
PROGRAM hii itahusisha muundo wa mpira wa miguu ili
kurahisisha uwasilishaji wa wazo kuu.
I.
Kocha.
II.
Refa.
III.
Vibendera.
IV.
Wachezaji.
Msimamo wa programu.
“kila mmoja ana jukumu la kushiriki kikamilifu kwenye
programu hii ili iweze kuleta matokeo chanya”
UFAFANUZI WA PROGRAMU
HII.
Ø Makocha.
Hili litakuwa Kundi la wanafunzi wenye uwezo wa juu kidogo au
zaidi ya wenzao kwa kila somo. Hii itahusisha kila somo mwanafunzi tofauti hata
kama mwanafunzi mmoja anaweza masomo yote peke yake.
Ø Refa.
Hili litakuwa ni Kundi la wanafunzi ambao watakuwa na kazi ya
Kukusanya maswali yanayohusiana na uhitaji wa wanafunzi wa darasa husika, na
kuyapeleka kwa makocha kwa ajili ya kuatatuliwa,
hivyo kila kabla ya kipindi maswali yanajibiwa darasani na kuwapa fursa
wanafunzi kujua majibu ya maswali yao. Na kama yatashindwa kwa
makocha(wanafunzi wenye uwezo) hapo ndipo yatapelekwa kwa mwalimu wa somo
husika.
Ø Vibendera.
Linesmens au vibendera huyu atakuwa ni mwalimu special ambaye
naye atakuwa na jukumu la kutatua matatizo madogomadogo ya program kama
upatikanaji wa chalk na pia upatikanaji wa majibu ya maswali ya vijana hawa.
Pia mwalimu huyu ndie atakaye kuwa na nafasi ya kutolea ufafanuzi wa program
hii ili kuhakikisha kila darasa lina program hii na hivyo kufanya uwezekano wa
kuendelea kwa program hiyo hivyo kuwezesha uendeshaji kwa ujumla wa program
hii.
Ø WACHEZAJI.
Darasa zima kutoa makocha na marefa, hili litakuwa Kundi la
wanafunzi lilogawanyika katika safu nne;
I.
Mlinda
mlango.
Itakuwa ni safu ya kukinga na kuondoa hatari zote
zitakazokuwa zikielekea kwenye program hii. Wanafunzi hawa wanapaswa kuwa wenye
busara, japo sio mara zote lakini mara nyingi ni wale viongozi wa dini zote,
waislamu na wakristo na dini nyingine.
II.
Safu
ya ulinzi.
Hawa watakuwa wanafunzi ambao
watakuwa na kazi ya kuibua maswali na njia au suluhu ambazo hazikueleweka na
darasa kwa ujumla,( hivyo aina ya wanafunzi hawa inatakiwa iwe ile ya wanafunzi
ambao ni wadadisi), wayarudishe maswali na suluhu hizo tena kwenye mdaharo na
kuwezesha kurudiwa ili kila mmoja aelewe.
III.
Safu
ya kati.
Hili
litakuwa Kundi ambalo linahusika na Kukusanya maswali ya darasani pamoja na
mitihani ya nyuma na kuigawanya darasani aidha kwa kuandika ubaoni au kwa
kugawanya karatasi na kuhakikisha utunzaji wa maswali mengine kwa ajili ya
wakati husika hapo baadae.
IV.
Safu
ya ushambuliaji.
Mwisho kutakuwa na Kundi la wanafunzi
ambao hawa watakuwa ni wenye kusimamia na kuangazia sheria za shule na pia hawa
watakuwa na kazi ya kuwashirikisha wanafunzi wa shule jirani ili kujipima uwezo
binafsi.
Hawa pia watakuwa wana kazi ya kutoa
vipaumbele vya kufanya wakati wa program hii, vinavyohusiana na muda sahihi kwa
kila shughuli.
NB; KILA KIPENGELE KILICHOPO
CHENYE KUHUSISHA WANAFUNZI KINAWEZA KUUNGANISHWA NA UONGOZI WA SHULE WA
WANAFUNZI.
MAPENDEKEZO.
Sisi kama afrotalent tunapendekeza “kuwa
na sheria ndogo juu ya Udereva wa bodaboda itakayozingatia umri wa madereva,
sheria za barabarani,kuvaa vifaa vya
usalama kati ya dereva na abiria”