#ANAITWA-ROMA
Popote ambapo utasikia aidha kwa kutegemea au kutotegemea neno "ANAITWA ROMA" Basi jua ni new hit song ya mwanamuziki na mwanaharakati kutoka Afrika ya mashariki yaani kutoka Tanzania, kwa jina la muziki kama ROMA. mara nyingi amaekua akitoa nyimbo ambazo kwa muda mrefu maudhui yake yamekuwa sio ya kisiasa kama nyimbo hii, hii inafuata baada kutoa hit song nyingine ya kijiwe nongwa akiwa amemshirkisha Ney wa mitego akiwa kwenye muungano wao yeye na stamina ambapo, wao kwa pamoja na Ney wa mitego wamekiumiza kinoma kwenye ngoma yao hiyo ya kijiwe nongwa.
but swali ni hili ni kweli kwamba vijana wawili hawa walio kwenye umoja huo Kama ROSTAM wamekwama kufikia tamaa au shabaha yao ya kufanya kila muziki pamoja, ni kweli kuwa stamina anogopa kuikosoa serikali kama ambavyo amekuwa akifanya roma mkatoliki kwenye wimbo wake huu mpya ambapo amemshirikisha msanii kinda aitwaye "one six"
ROMA MKATOLIKI NA KIU YA USHINDI.
Roma mkatoliki kama wasanii wengine wa hiphop naye pia amekuwa akinukuliwa kwa kutabiri matukio ambayo kwa kiasi fulani yamekuwa yakitokea kiukweli na kuwaacha watu midomo wazi.
Akiwa nchini marekani, Roma alisema kuwa sio matukio yote anayoyaimba yanamfanya yeye awe kama nabii la hasha bali ni baadhi ya matukio hayo kuwa kweli yako kwenye jamii yetu kitu ambacho kinaweka wazi nini cha kuimba na nini sio cha kuimba kiliripoti kituo kikubwa cha media ya habari cha VOA swahili.
kwa namna yangu ya kuyaangalia mambo nadhani huu ndio muda sahihi kwa msanii kama roma mkatoliki kutwaa tasnia ya muziki wa hiphop hasa hiphop ya kisiasa kama anayofanya sasa na pale awali alipokuwa akifanya kazi zake za uimbaji.
picha na google.com//roma mkatoliki.