MAWAZO YAKO MTAJI WAKO ILA MPAKA UWASHIRIKISHE WATU WENGI

Kipi bora, kufa wakati ulikuwa na mpango wa kuendeleza kuishi au kuishi wakati ulikuwa na uhitaji wa kufa, labda naweza kuwa kati ya wale wachache usiowafahamu ambao wamekuja kwako na kutoelea tonge kwenye Tamu na chungu zako na kukupa tonge hilo ili uionje radha halisi ya nini na kwanini unapaswa kusimama wewe kama wewe na kwa mwongozo upi ulio bora ambapo kila mtu anaweza kujifunza mambo hayo kutoka kwako.
E bwana, hujachelewa kuelewa, kwani walio wengi wanaweza kukupa neno la ziada na kufungua uelewa wako ambao kwa sasa yamkini umefungwa na mawazo ya mafanikio lakini yakikosa namna sahihi ya kukusanya mafanikio yako, na kiukweli inaonekana kama umekubali matokeo kiasi hauwezi kuupokea ushauri sahihi hata kama unaweza kuwa sawa na sahihi kwajili yako tu, lakini kingine ni kuwa waliokuwa wanaonekana kama ni wale ambao umekuwa ukiwaamini wameshindwa kufanana na ulivyodhani yaani kukuelemisha namna  wamefika pale walipo sasa.
USIJALI…KWANI Habari njema ni kuwa hakuna umri au wakati wa mwisho wa mafanikio ya mtu, mfano, kwa kuwaangalia maraisi wa USA kama TRUMP na OBAMA utagundua kitu ambacho namaanisha, hapa ni kuwa TRUMP ana umri mkubwa sana na sasa ni raisi wa USA na upande wa OBAMA amekuwa raisi ndani ya mihula miwili, ambapo karibu muongo mmoja ameongoza, hapa swali la msingi ambalo unapaswa kujiuliza ni kuwa je? Kuna wakati hata mmoja ambapo mtu yoyote aliyewahi dhani mtu mwenye umri mkubwa kama DONALD TRUMP angeweza kuwa kiongozi wa USA.
Tafsiri sahihi ya nini na kwanini, inatokana na nani aliyekutwa kadhia hii (yaani kifupi, mtu anayekuwa na wazo ambalo anaona haliwezi kufikiwa kutokana na majibu aliyonayo yeye mwenyewe) 
Zifuatazo ni njia sahihi za Kuwezesha mtaji wa mawazo yake ili aweze kuja na njia sawasawa ya kuyafanikisha;
01.-KUACHA UBINAFSI-
Kuwa na wazo na usiwaambie wengine kuna uwezekano mkubwa wa kutopata namna mapya na pengine kutojua jinsi ya kupata mtaji au kutojua wapi biashara au shughuli yako inaweza kufana/kusitawi. Kuto shirikisha jamii yako inawezekana kabisa wewe ukawa na ubinafsi kiasi Fulani kitu ambacho kinawezafunika mafanikio yako ya hivi karibuni, au siku za usoni
EBWANA TUKUTANE WIKI IJAYO ILI TUENDELEEE KUPEANA MA INFO YA KIJANJA.
Tu follow kwenye platform zetu zoote 
IG brightermango
FB Brighter Mango
Twitter GwemelaM
Facebook page Brighter Mango

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post