MAPITO YANAPITA KWENYE MAISHA YETU NA SIO SISI TUNAYAISHI KWENYE MAISHA YETU.

MAPITO YANAPITA KWENYE MAISHA YETU NA SIO SISI TUNAYAISHI KWENYE MAISHA YETU.
Za Mizunguko hapo ulipo?
Najua uko unapambania kombe lako, we kaza na endelea kulipambania kiongozi.
Fikiri kidogo kuhusu hili " Mapito ni nini?"
Mimi naamini kwanza mapito ni mambo Magumu maishani mwetu, pili haya magumu hatuyapitii kwenye maisha yetu yote, bali yenyewe ndio yanapita kwa muda tu maishani mwetu....nahisi ndio sababu hata yenyewe huitwa  Mapito. 
HAYAKUJA KWAKO KUISHI MILELE, ILA YATABAKI KWAKO KAMA TU UKIYAKARIBISHA KWA KUTOJIPANGA KUYAONDOA, 
IVI unafahamu kuwa umaskini, njaa, ukosefu wa huduma za afya, usimamizi mbovu wa mambo na hata ukiukwaji wa sheria, pamoja na uonevu vyoote na vitu kama vile utasa, ugumba na vifo au mauiti yoote ni mapito.
JUA JAMBO HILI, USHUHUDA WA MAMBO HAYA KUWA YAMEPITA BAADHI YAKE UNAO.
NINI KIFANYIKE ILI TUSIJEYAKARIBISHA NA KUWA YA KUDUMU MAISHANI MWETU.
🌱Kwanza Amini yanapita maishani mwako na sio wewe unaeyapitia katika haya maisha.
🌱Pili ujipange kwa habari ya kutosahau ahadi au mipango uliyonayo.
🌱Kwa imani yako aidha muislamu au mkristo waweza mtanguliza M/Mungu kwa kuwa Imani ina ambatana na ushuhuda au vitendo iki kwamba uweze kuyaona yaliopita awali.
🌱Usifiche mapito yako ukaumia, na wala usiwatangazie watu kwa nia ovu.
🌱Andika namna bora ya kuliepuka pito hilo unalokuwa umesha lishinda kwa wakati fulani.
Shukrani za pekee kwa @Paul_Clement na kwa Masomo haya hususani kwa wale wenye lengo la kujifungua kifikra unaweza niandikia katika
Barua pepe yangu👉brightermango012@gmail.com
pia waweza nitumia ujumbe kwenye fb account yangu.
usishau ku share kazi yangu hii ili niweze kuongeza familia ya wasomaji.
Mwisho ninawapenda Nyoote.
MUNGU AWALINDE POPOTE MLIPO.

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post