KILA MTU ANA AKILI SAWA NA MWENZAKE... HII NDIO TOFAUTI YA KWELI KATI YA TAJIRI MSOMI NA TAJIRI AMBAYE HAJASOMA
GWEMELA
BLOG brightermango.blogspot.com
tsapp +255674167126
Insta @brightermango
JE? nawewe pia umesahau... ya kwamba kila mtu anayo akili sawa na mwenzake.
Je? Huoni tena thamani ya maamuzi sahihi uliyoyachagua yanavyokupaisha juu?
Je? Hukumbuki nimeshapiga kelele vya kutosha kukuambia ya kuwa akili ni maamuzi?..
Sasa ikiwa ni akili mbovu... basi hapo yamaanisha maamuzi yasiyo sahihi.. na ikiwa maamuzi sahihi basi ina maanisha akili njema.
Kwa hakika kila aliyeko duniani ana akili sawasawa na mwenzake.... mfano, Watu wawili wakifundishwa nini ni kijiko na nini ni kisu alafu woote wakaagizwa kuchukua kisu mahali vilipo ... mmoja akaleta kisu na wa pili akaleta kijiko
yaelekea yule aliyeleta kisu akawa na akili na wa pili akawa kakosea yaani akawa hana akili.
USHAHIDI HUU NDIO UNAOSEMA KWANINI MTU AMBAYE HAJASOMA ANAWEZA KUWA TAJIRI.. KWANI AKILI NI MAAMUZI SAHIHI NA ELIMU YA MADARASANI INAHUSISHA KUMBUKUMBU...
Na ndio sababu wasomi ni wengi bila mafanikio... kwani walio wengi wanakosea maamuzi...
FAIDA YA KUMBUKUMBU KWENYE AKILI NI kukupa uwezo wa kufanya maamuzi hata wakati wa baadae... ndio sababu au tofauti iliyopo kati ya aliyesoma na ambaye hajasoma.