HIVI UNAFAHAMU KUWA❓
"HATA MWIZI UNAYEMKAMATA BAADA YA KUKUIBIA, NA YEYE PIA ALIKUWA AKIKAMILISHA FURAHA YAKE, SEMA TOFAUTI NA WEWE, YEYE HAWEZI KUVUMILIA MAUMIVU NA KUKUSANYA KIDOGO KIDOGO NA KWAHIVO ANATUMIA NGUVU KUBWA AKILI MBAYA ILI KUPATA PESA AU MALI NYINGI KWA WAKATI MFUPI BILA YA UCHOVU AU MAUMIVU"
matokeo yake yako wazi... Akikamatwa hupatiwa maumivu aliyoyakwepa na hata huchoshwa sana. Kiuhalisia inasemekana kuwa mtu yeyote anayeishi anadhulumu kwa kiasi fulani nafsi au vitu vinanvyomzunguka. Kwa mfano hewa tunayovuta huwa tunaigombania na ndio sababu mapafu yetu hupanda na kushuka IKIWA NI ISHARA YA USHINDANI.
Kwenye utajiri pia, ili mmoja awe maskini, ni lazima yule aliyetajiri amfanye maskini asiwe na elimu...maarifa na zaidi awe na utiifu kwake...kitu ambacho kinafanya sisi kama jamii tuone sawa japokuwa si sawa na ama hakika Mabadiliko ya lazima yanahitajika haraka kwenye jamii yetu.
TATIZO KUU.
"KWENYE JAMII YETU KUNA VITU WAMESHAVIKUBALI NA KUONA VIKO SAHIHI, JAPO KI UHALISIA BAADHI HAVIKO SAHIHI, HII NDIYO WATU HUITA DESTURI... Kwa kawaida watu hukimbilia kusena kuwa "hii ndiyo desturi yetu.." ili wakamilishe malengo yao"
Jamii inalazimisha kuwa,
Maskini haruhusiwi kupata elimu.
Maskini hawezi shiriki maamuzi.
Maskini hapaswi kuonekana sehemu za wazi eti aibu
Maskini eti Ni mtumwa wa tajiri.
Maskini ni wa kukosa haki mahakamani.
Wakati si sahihi na wala si sawa.....
Nafikiri wakati umefika sote tubadilike na kufanya maamuzi sahihi.
Niko natamani wote Tuinuke.... TAJA MAMBO YOYOTE unayohisi jamii imeshayakubali yanayokuathiri kiJAMII NA KIUCHUMI..
TEMBELEA BLOG YANGU GOOGLE KWA KUANDIKA Brightermango...itakuja blog yangu ya kwanza.
imeandikwa na Gwemela Conrad.
CEO.
Brightermango.
photo credit [[ Mary S. Mtui&friend]]
Like my page Brightermango purpose