MAMBO MANNE (4) YA KUACHA ILI UWE MSHINDI.

Na,

Brightermango.


MAMBO 4 YA KUACHA SASA ILI UWE MSHINDI. 

1. ACHA KUANDAMANA NA WATU WASIO SAHIHI.

Maisha haya ni mafupi kiasi kuwa kama tutaruhusu namna yoyote kuwa na watu ambao muda mwingi wanakurudisha nyuma haiwezi kamwe kuwa sawa au na usaidizi badala yake tutaambulia hasara kubwa. Ishara ya wazi  ya watu hao, mara zote wana kuwa na wewe kwenye muda wako wa juu wa mafanikio lakini ukianza kushuka hutomuona yeyote kati yao.

  Anza kuandamana na watu sahihi: hawa ni wale tu ambao wanatambua mchango wako na kuelewa zaidi hata kama hujawaeleza kukuhusu.


photo: Employment page.


2. ACHA KUKWEPA AU KUKIMBIA MATATIZO YAKO.

Saa chache unapokutana na tatizo huwa unapatwa na hofu... lakini kumbuka kadiri unavyojiimarisha zaidi katika kutatua changamoto ndivyo unavyokomaa kukabili nafasi za juu na kubwa hapo mbeleni aidha kwenye ajira au binafsi.

...Jaribu sasa kupambana nayo; Ukweli ni kwamba hata kama ungepaa juu zaidi na kuishi huko ulikokwenda huwezi kukwepa matatizo yanayokuhusu wewe pekee.

kuyatatua matatizo yako kuna andaa namna mpya yako na ziaidi kama utazitatua sawasawa basi utafikia hatua ya kuwa wewe ni bora sana.

Kuna watu wanasema " Heri nusu shari kuliko shari kamili" lakini hapa ili ubaki mshindi usikwepe matatizo yako zaidi wewe pambania kwenda mbele.

Hakikisha unatatua matatizo yako ili uwe imara zaidi kuelekea hatua ngumu zaidi.


3. ACHA KUJIDANGANYA.

Kuwa mkweli na muwazi ni kazi ngumu sana kwa mwanadamu ambaye kila wakati anatamani kuwa na thamani hapa duniani kitu ambacho kinafisha utu ule wa ndani tulio nao kiasili na hivyo kupelekea mambo mengi tuzidi au tuendelee kujidanganya.

Uongo mwingi upo hapa.. kwenye hali ya kimaisha, ukwasi na pia imani.

Maswali muhimu unayopaswa kuyakumbuka ni

 1. Je? niliyoyasema leo ni kweli.

 2.Ni kweli kwamba niko sawa kwa hili ninalolifanya.?

 3 . Hivi ninavyoonekana hapa hadharani ndivyo ninavyojiona nikiwa peke yangu?

4. Mara ngapi nimetengeneza furaha au chuki kwa watu wanaonizunguka?

...Anza Kuwa muwazi na mkweli kwako, jiambie nini kiko sawa kwako na nini hakiko sawa kwako.. watu wanapoamua kuruhusu fikra chanya basi ndipo wanapokuwa washindi.

photo from: pinterest.

4. ACHA KUYAWEKA MAHITAJI YAKO NYUMA.


Kama hujui kitu kinachouma sana ni vile unavyopotea wewe kipindi unataka kumfurahisha mwingine. ukiweka mbele maisha yako haina maana wewe ni mbinafsi.. Ebu fikiri hili... kama ukiweka nafasi ya mbele mafanikio ya rafiki zako, ni lini utafanya au hata kufikiri kuhusiana na vitu vinavyoweza kukufanikisha. Yapo ambayo labda huyajui.. kwa kawaida watu huyahesabu mafanikio katika kona zao binafsi... wapo wanaamini ni kutembea dunia nzima, wengine kuwa ni kuoa mwanamke mrembo zaidi, wengine wanaamini ni kuwajengea msingi mwema watoto au wazazi wao wa kimaisha na lakini zaidi wengine mafanikio yao wengine ni kuwa na ukwasi au fedha nyingi.



Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post