ZIJUE FAIDA ZA KUKOSOLEWA KWENYE MAISHA YAKO.
MWANDISHI NI Gwemela Conrad Michael.
NAMBARI YA SIMU NI 0674167126.
Vitabu vya nukuu ni,
" Building a Peaceful Nation : Julius Nyerere 1960-1964 " by BJERK Rochester University Press. U S A.
" THE ART OF THINKING IN SYSTEMS : By STEVEN SCHUSTER"
Mnamo mwaka 1964 Januari 19, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Baadhi ya wanamapinduzi wa Zanzibar, Kama wakina John Okello walikuwa wamekaa wakiwaza jinsi ya kuiletea amani ya kudumu Zanzibar... hii ikiwa ni baada tu ya wiki kupita tangu baadhi ya watu waliokuwa wakimpinga #MzeeKarume kutaka kufanya mapinduzi.
Swali Gumu la Mwalimu lilikuwa ni " Je? ni kwa jinsi gani angeweza kuwapatia majirani zake amani ya kudumu, hasa kwa kipindi hicho mwalimu alikuwa anapokea sana maombi ya kutuma misaada ya dharula huku wakuu wa Zanzibar wakiwa wanamtembelea sana Mwalimu, Akiwemo Karume, Hanga, na Babu.... na kwa kipindi chote hiki walikuwa Tanganyika haijaungana na Zanzibar" Building peaceful nation by BJERK-2015.
Baadhi ya watu walimshauri Mwalimu aungane na Zanzibar ili iwe rahisi kiusalama na baada ya muda kupita Mwalimu alikubali kubadilika... kutotoa msaada zaidi na badala yake kujenga undugu.-Bjerk 2015.
LENGO KUBWA HAPO.
Lengo la Nukuu hiyo hapo Juuu ni kWamba, Mpaka sasa tuko na Amani ya kitaifa(hakuna vita) Kwa kiasi kikubwa ni kutokana na Misingi ya Baba wa taifa hili, ambapo kwa jinsi alivyokuwa, inawezekana kabisa alikuwa mtu wa kupokea masahihisho kwa moyo wa dhati.
Ndio sababu leo hatuko kwenye transit camps, na ndio sababu leo hatujawa bullied nchi nyingine, na ndio sababu leo Yeye Baba Wa Taifa ndie SUPERSTAR WA KILA RIKA NA MOST CELEBRATED PERSON... kwa UFUPI TU, yeye ndio Mfano halisi wa kukubali kukosolewa ili ufanikiwe.
TAFITI...
Kwa Mujibu wa kitabu cha " THE ART OF THINKING IN SYSTEM" alichoandika Bwana Steven Schuster, anasema "Ukikosolewa mara kadhaa unabadilika kutoka namna ile uliyokosolewa na kukufanya uwe unafikiri sawasawa"
HITIMISHO.
Hakuna uwezekano wa mtu Kufikiri sawasawa pasipo kukosolewa... Kubali kukosolewa.. itakusaidia kukabili changamoto Kubwa Maishani Mwako.
Like ?Brightermango purpose.
Join group langu lBrightermango.