KWA WALE WACHACHE TUNAWEZA KUJARIBU HUKU...
PART 2: SOMO LA FOREX.
MISAMIATI / LUGHA KWENYE FOREX
Kikawaida kwenye kila fani au sekta hapakosekani kuwa na misamiati au lugha ambayo inapachikwa pale ili krahisisha mawasiliano. Mfano kwenye fani ya udereva basi pale kuna lugha ya ishara ambayo inawasaidia madereva kuwasiliana pindi wawapo barabarani, mahakamani pia kuna lugha ambao itasaidia kusaidia mawasiliano, migahawani pote huko kuna ligha zake... mfano muuzaji anaweza kuuliza " Nani sambusa? alafu wewe ukajibu " MIMI" tena kwa sauti. sasa je, wewe ni sambusa?😂 Hapana wewe sio sambusa ila umelazimika kuendana na lugha ya scheme husika.
sasa basi kwenye FOREX pia tuna misamiati ambayo imewekwa ili kutusaidia kwenye mawasiliano/mazugumzo.
1)BEAR / BEARISH / SHORT
Bear ni mnyama amaepatikana hasa bara la ASIA kwenye maeneo yenye baridi sana. ni mnyama ambae akitaka kukushambulia basi atanyanyuka juu kisha atakupigiza kwa kichwa chake kwenda chini. kwenye forex neno BEAR linaendana pia na maneno BEARISH & SHORT ambayo yote kwa ujumla yakimaanisha SELL. sasa mtu akikwambia EURUSD ni BEARSH maana yake ni kwamba EURUSD ina SELL au inadondoka chini.
2)BULL / BULLISH / LONG
Bull ni ngombe, ni mnyama anaefahamika sana duniani kote.. asili ya mnyama huyu akitaka kukushambulia basi anakufwata kisha anakuchota kwa bichwa lake ambalo limepambwa kwa pembe zilizokomaa mithili kokoto.. basi anakupigiza kwa mtindo wakukuchota nakukupeleka juu ( usiombe ukatane na hili sebene maana binladen mtoa roho lazima akukatie tiketi yakwenda peponi😄)
Sasa basi kwenye forex meno BULL, BULLISH, LONG linamaanisha kwamba BUY yaani pair fulani ina BUY au inakwenda juu.
🥳. LONG/BULLISH📈
Hii ni termonology ambayo unasikia watu wakiiongelea. kama imepatikana opportunity ya kulong/bullish hapa maana yake NUNUA. Bull ni aina za mnyama ambae anakula majani hivo candlestick zake nyingi zinakuwa zikiwakilishwa na rangi ya kijani. Huyu mnyama akitaka kukudhuru huinamisha kichwa chini na anakunyanyua kwa kukuchota kukupeleka juu. Hivyo katika Forex hapa inamaanisha soko linatoka chini linapanda juu.
🥳. SHORT/BEARISH📉
Kama imepatikana opportunity ya kushort/bearish hapa maana yake UZA.. Bear ni aina ya mnyama ambae anakula nyama, hivo candlestick yake huwakilishwa na rangi nyekundu. Huyu mnyama anavyokudhuru huruka juu kisha hukushusha chini. Hii katika forex inamaanisha soko linatoka juu kushuka chini.
EXCHANGE RATES
Sababu sarafu zinatrediwa in pairs and exchanged kutoka sarafu moja kuja nyingine unapotrade. Rate unavyokua unafanya exchange tunaita exchange rate. Sarafu kubwa zinatradiwa against dolla ya marekani (USD) ambayo ndio sarafu inayotrediwa zaidi ya sarafu yoyote. Sarafu zinazofuata kwa kutrediwa zaidi ni euro (EUR), yen ya japan (JPY) , pound ya uingereza (GBP) na Swiss Franc (CHF). Na pindi sarafu hizi nne zinapokuatana na dolla ya marekani hutengeneza pair tunazoziita major pair. Na karibuni dolla ya Australia (AUD) pia inatamkwa kama inaweka muunganiko wa major pair.
Sarafu ya mwanzo iliopo kwenye pair huitwa base currency na sarafu inayokaa upande wa pili huita Counter au Quote currency. Exchange rates hufafanua ni kiasi gani cha quote currency kinatakiwa kulipwa ili kupata unit moja ya base currency.
🙌🏻. BASE CURRENCY
Hiki ni kiini msingi katika kununua au kuuza katika forex. kama utabuy USD/JPY Hii ni kumaanisha unanunua dola ya kimarekani na wakati huohuo unauza yen ya kijapani.
Kwa maana nyingine Base currency in fedha unayoitumia wewe
Kwa mfano sisi Tanzania base currency yetu ni shillings
Kwenye Forex utatambua base currency kwa kuwa inakuwa ya kwanza kwenye pair mfano USD/JPY
Hapa USD ni base currency yako
🙌🏻. QUOTE CURRENCY
Hii ni ile sarafu ya pili katika pair ya sarafu husika unapofanya trade. Mfano USD/JPY, JPY ndio quote currency.
Katika Biashara ya forex Trading kuna Aina za Matrader...Nazo ni 👇🏾👇🏾
1. Scalper
2. Intra day trader
3. Swing trader
4. Positional trader
1. SCALPERS
Hawa ni aina ya matrader ambao hukaa sokoni kwa muda muchachee sana pia hutumumia timeframe ndogo kuanzia 30 mins had 5mins kuingia kwenye trade, aina hii ya matrader ni aina ambayo haimruhusu trader kuhold kwa muda mrefu kutokana na timeframe zinazotumika kutoruhusu trade kuholdiwa. maranyingi scalpers huchukua pips 10 had pips 30 kisha hutoka kwenye market.
2. INTRADAY TRADER
hili ni kundi la matrader wanaoingia sokoni kwa siku au masaa kadhaa na kutoka na kundi hili limebeba trader weng katokana na matrader weng kutopenda kulala wakiwa wame hold trade na mara nying kundi hili utumia time frame ndogo kama 30mn 1hr au 4hr
3. SWING TRADER
HaWa ni aina ya trader ambao ukaa kwenye soko zaidi ya siku moja na mara nying hawa utumia time frame kubwa kuanzia masa 4 na kuendelea na aina hii utumiwa na matrader ambao wana uzoefu katika soko
4. POSITION TRADER
Position traders ni matrader ambao hukaa kwa muda mrefu zaidi sokoni kuliko matrader wote, hasa hukaa sokoni kuanzia mwezi na wanaweza kuhold hadi miezi 3. hii ni aina ya trading ambayo unarisk kidogo kwa kupata kingi zaidi.. mfano unaweza kurisk $50 ili kupata hadi $800 kutokana na muda utakao hold
TAKE PROFIT
Baada ya kuuza au kununua katika soko hauna haja ya kukaa kwenye chart unaitizama ifike idadi ya pips unazohitaji, Hivyo utaweka oda ya kujifunga pindi price au soko litakavyofika kwenye pips unaohitaji kama faida, Oda hio au hilo eneo huita Take profit
STOP LOSS
Unavyotrade lazima ujue katika hii trade yangu kama market haitaenda kama nilivyotarajia basi ikifika eneo hili trade hii itakua ni invalid. Eneo ambalo trade yako unaona ikifika trades hio itakua Invalid eneo hilo linaitwa STOP LOSS. Eneo ambalo ni ukomo wa hasara isiendelee.
UCHAMBUZI WA SOKO:
Kuna aina kuu tatu za kuchambua soko ( Market analysis)
1. Technical analysis
2. Fundamental analysis
3. Sentimental analysis
TECHNICAL ANALYSIS
Huu ni aina ya uchambuzi wa soko kwa kuangalia mwenendo wa bei kupitia charts ambapo tunaangalia jinsi bei (price) ilivyotembea wakati uliopita na tabia ilizoonesha na tunahusianisha na wakati huo inavyotembea ili tuweze kutabiri/kutambua wakati ujao itaelekea wapi.
FUNDAMENTAL ANALYSIS
Huu ni ufanyaji wa biashara kwa kuliangalia soko kulingana na shughuli za kiuchumi,kisiasa na kijamii ambazo hupelekea kuleta madhara katika suala zima la demand and supply
2. FUNDAMENTAL ANALYSIS
Huu ni uchambuzi unaozingatia kwa kuangalia matukio mbalimbali yanayoendelea kwa wakati husika, mfano taaarifa za ongezeko la ajira au kupungua katika mataifa makubwa kama USA, au mvutano wa kiuchumi kati ya china na marekani. Hive hayo matukio yanaweza kusababpisha sarafu kupanda au kushuka thamani kwa kasi sana.
3. SENTIMENTAL ANALYSIS
Hii ni nia ya uchambuzi unaousisha kuchukua taarifa au analysis zilizofanyika kutoka kea matrader mbalimbali mfano uliowafollow kwenye social media ivyo unazikusanya na kufanya maamuzi ya jumla, na hata sio njia nzur kama kweli umewekeza pesa yak katika biashara hii ya forex
PIP (PERCENTAGE IN POINT)
Hiki i kiasi cha thamani kinachocheza kulingana na mzunguko wa sarafu husika katika biashara. Huanza kuhesabiwa kutoka desimali ya nne katika pair mfano thamani ya USD/CHF ni 1.1379, thamani hii ikimove toka 1.13*79* mpaka 1.13*80* hapo inakuwa ni 1 pip
Isipokuwa kwa pair inazohusisha sarafu ya YEN nafasi za decimal zitakuwa tatu na sio nne kama pair nyingine. Mfano USD/JPY=1.137 hivo pip unaanza kuhesabu kwenye 7
Faida au hasara kwenye Forex Trade zinapimwa kwa PIPS.
Kitefu chake ni "Percentage In Point". Pip ni tofauti ya POINT MOJA katika bei ya Pair ya Currency tokea ulipoweka ORDER yako. Its a 1point Price Movement ama kwenda juu au kuja chini.
Hii tofauti ya bei (Pip) inapimwa katika viwango vya Desimali. Currency Pairs nyingi (sio zote tafadhali) zinatumia SEHEMU NNE ZA DESIMALI. Utakuta kwenye Platform wanaandika SEHEMU TANO lakini ni ili kukusaidia wewe mfanyabiasha, ila zinazohesabika ni NNE.
Utaelewa vizuri kwenye mfano. Chukulia hiyo ya pale juu:
EUR/USD = 1.25358
Tunaangalia "Price Movement" katika sehemu ya 4 ya desimali. Ile ya tano inakupa tu sehemu ya Pip.
Chukulia hapo bei ibadilike ama kwenda juu au chini kama ifuatavyo:
EUR/USD = 1.25458
⬆
EUR/USD = 1.25358
⬇
EUR/USD = 1.25258
▶️ Kutokea 1.25358 kwenda 1.25458 maana yake bei imepanda kwa 10pips.
▶️ Kutokea 1.25358 mpaka 1.25258 bei imeshuka kwa 10pips.
Swali, je kutoka 1.25258 mpaka 1.25200?
Jibu, imeshuka kwa 5.8pips. Sawa mpaka hapo?
Kwa hiyo, FAIDA na HASARA katika Forex zinapimwa kwa PIPS. Ukiwakuta watu wanaambiana, mimi leo nimepata, 30 USD, 50 Yen, 70 Paunds...unajua tu hawa sio professionals. Kule watu wanajisifia Pips sio Dola au Paundi au Yen. Utakuta mtaalam anasema, Mimi ninapata Average/Wastani wa 500Pips, au 700Pips au 1100Pips kwa wiki au kwa mwezi, nk. Sio Dola! Na mtaalamu anayependwa na wateja,..Anayeaminiwa kwamba anao uwezo wa Market Analysis mzuri ni yule anayejikusanyia PIPS nyingi mwisho wa siku.