Forex inasimama badala ya neno FOREIGN EXCHANGE, Ambapo unakuwa unabadili sarafu moja toka sarafu nyingine. Mfano kama ukitoka Tanzania unatumia TSH ukaenda Kenya ambapo wanatumia KSH itakubidi ubadilishe sarafu yako ya kitanzania kwenda katika saafu ya kikenya. Kwa zoezi hilo unakuwa umeshafanya FOREX.
Kubadilisha hela huku mtandaoni ni biashara ambayo inazungusha hela nyingi kupita aina yoyote ya biashara ulimwenguni kwa siku. Kwa siku biashara hii mzunguko wake wa hela ni zaidi ya $5 TRILLION. Wakati stock exchange ya New York kwa siku ni $22.4billion, Tokyo ni $18.4 billion na London ni $7.2 billion kwa siku. Na hizo ni stock exchange kubwa duniani, hivo FOREX ONLINE ni kubwa kuliko hizi stock exchange.
Biashara hii mara ya kwanza ilikuwa ikifanywa na Institution kubwa za kifedha kama benki kuu za nchi na mabank ya kibiashara. Lakini kulingana na mapinduzi ya kiteknolojia hata wewe sasa unaweza kuingia katika hii biashara kutokana kuwepo na mtu wa kati ambaye unaingia kwenye soko kupitia yeye. Huyu anaitwa BROKER. Unafungua kaunti kwake unaingiza kiwango cha mtaji unachotaka kuanza kufanya nacho biashara
Watu gani wanaokuwepo/wanaoshiriki katika hii biashara?
1. Benki kuu (Central banks)
2. Serikali (Government)
3. Umoja wa wawekezaji(investment coorperation)
4. Wafanyabiashara wa duniani kote(businessies worldwide)
5 Wafanyabiashara wadogo(Retail trader)
FAIDA ZA FOREX
1. Una uwezo wa kufanaya biashara sehemu yeyote ulipo
2. Unaweza kutoa faida hela zako mda wowote ndani ya siku za wiki.
3. Sheria rahisi.
4. Inapatikana masaa 24
5. Uwiano mzuri kwa kiasi kidogo unaweza ingiza faida kubwa. (Leverage)
6. Upatikanaji wa FAIDA kubwa na kwa haraka.
Kweny Forex ili uweze kuifanya inakuhitaj uwe na MTU kati (ambae kweny hii biashar tunamuita Broker)
Mfano mzur nikama vile unataka kuanza kutumia simu kwa Mara yakwanza silazima uangalie ni line gani IPO vzur iwe Tigo,voda,halotel nk sindio? So nakwenye Forex napo IPO ivyo lazima uangalie broker gani mzur na mwenye makato madogo na mwenye njia nyepesi zakutoa ela nakuweka ili umtumie
BROKER NI NANI?
Kwakifupi broker ni kama bank yako ya mtandaoni, Yaani ili uweze kushiriki kwenye market lazima upitie kwa broker... Broker anatuwezesha mimi na were (RETAIL TRADERS) kuweza kushiriki kwenye FOREX MARKET kutokana na mitaji yetu kuwa midogo na kutoweza kushiriki moja kwa mooja kwenye FOREX MARKET. ieleweke kwamba retail trader yeyote lazier apitie kea broker ili kuwezeshwa kushiriki kwenye FOREX MARKET.
JE BROKER ANATUWEZESHASHE KUSHIRIKI KWENYE FOREX MARKET?
Broker anatuwezesha sis kushiriki kwenye market kwa kupitia kitu kinachoitwa LEVERAGE.
LEVERAGE huu ni kama mkopo ambapo broker anakuwezesha ili uweze kuingia sokoni
MAMBO GANI YA KUZINGATIA UNAPOMCHAGUA BROKER.
Kabla hujachagua broker kuna factor inabidi utazame maana kuna brokers weng scams
1. Spread
2. Commision and fees
3. Urahisi wa utumiaji wa trading platform ukiwa chini yake.
4. Kiasi cha chini unachoweza kudeposit
5. Gharama zozote za ziada kama zipo
6. Control juu ya matukio mbalimbali yanapotokea dhidi ya position yako
7. Platform gani unaweZa kutumia ukiwa chini yake
8. Urahisi wa kudeposit na kuwithdraw
9.Msaada wa huduma kwa wateja
9. Ana reputation gani, kama ana partner na taasisi ip inayoaminika.
10. Management yake nzima, oFisi zake na namna ya kumfikia kama ana fikika.
Ukitak kufungua Account kwa Broker yeyote unahitaji kupitia vitu hivi👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
1.kujisajiri (sign up)
2.kufanya verification(Hapa utaambatanisha Document zako muhimu kama National I'd,Kadi ya mpiga Kura au license kama unayo kweny kufungua real Account)
3.kufungua account
''We believe, life is only a gift that expires and success in anything we have is not ours, its for human kind and so our wisdom''
-Gwemela