SERIKALI IPUNGUZE KUTOA UFAFANUZI...WAJE NA SULUHU YA MAKATO YA MIAMALA.

ANAANDIKA THADEO OLE MUSHI KUHUSU MAKATO.
SERIKALI IPUNGUZE KUTOA UFAFANUZI WAJE NA SOLUTION. 

Na Thadei Ole Mushi.
Tweet kitoka kwa makamo wa raisi.



Viongozi wetu tunawapenda Sana, tunalipenda pia Taifa letu Sana, tunahitaji kulijenga Kwa Hali na Mali lakini hili la Tozo za miamala tunaweza kulirekebisha bila kupanua mjadala huu Kwa jamii. Nimeona tweeter hii inayosemekana ni ya Makamu wetu wa Rais nimetafakari Sana.....

Mwaka 1879 Malkia aliyekuwa anaiongoza Ufaransa Bi Marie Antoniette aliambiwa wananchi wake hawana Mikate akajibu kwa kifaransa “Qu’ils mangent de la brioche” kwa maana ya kiingereza “Let them eat cake" kwa kiswahili kisicho rasmi Sana ni kuwa Waambie wale Keki. 

Inatajwa kuwa Brioche waliyoambiwa wale kilikuwa Chakula Cha matajiri Sana Ufaransa, ambacho kwa walalahoi wa Ufaransa walikuwa hawawezi kukinunua ndio maana walikuwa wanahitaji mikate. Baada ya kauli ile Kutoka Malkia alipinduliwa na wananchi wenye hasira Kali. 

1. Mimi nadhani kwenye hili la Kodi ya miamala makampuni ya Simu wanachukua Fedha nyingi Sana. Serikali wakae nayo waone wanaganaje hiyo faida na makampuni hayo. Kiasi anachochukua wakala wa Simu ni Kidogo Sana. Mfano kwenye Shilingi 50,000 kwenye Moja ya kampuni Fulani Wakala analipwa Kamisheni ya Shilingi 200 tu wakati Kampuni la Simu wakichukua karibia 4,000. Serikali inaweza kuomba nusu ya hizi Fedha toka kwenye makampuni hayo. 

2. Kwa kuwa lazima tulipe Kodi na mm sikatai hili Ongezeko la hii Kodi kwenye miamala hesabu ifanyike ipunguzwe angalau pale tulipokuwa kabla tuongezee hapo Kidogo  ambacho hakitaleta hizi kelele huku mtaani.

3. Sio lazima Sana tuwe na makadirio Yale ya 1.5 trilioni kwenye hili la miamala Kwa mwaka mmoja. Tupunguze haya makadirio tuseme Kwa mwaka Huu wa Fedha tukusanye nusu ya makadirio haya halafu tutakusanya hiyo nyingine mwaka unaofuata. 

4. Bado wazo langu la kuanzisha shindano la ubunifu wa vyanzo vya mapato liwepo. Kwa watu Milioni 55 plus wa Tanzania hatukosi akili za kutupatia vyanzo vingine vipya vya mapato. Tusitegemee tu Hawa walioajiriwa kufanya Kazi hiyo tuwe na Flexibility ya kutafuta ku exploit mawazo ya Watanzania wote. 

5. Chama changu CCM kinapaswa kusimamia hili na kusema neno, madhara ya yote haya yatakuja kuadhibiwa CCM na sio Chadema. Kisiasa CCM inawajibu wa kutuliza Hali ya mambo na joto lililopanda kuliko Serikali.

6. Hii issue imegusa kila mtu kwenye nchi hii, Sasa hivi hata Mzazi asipotumiwa Fedha huko Vijijini Serikali ndio itakayotupiwa lawama. Yaani hata wazee wetu huko migombani ambao hawamiliki kibanda Cha M-Pesa wanaingia kwenye mgogoro huu Moja kwa Moja.

7. Mh Mwigulu Nchemba  asisubiri aitwe na Mh Rais, awahi Mwenyewe Ikulu kumweleza reaction ya huku mtaani na way foward. Kwa jinsi hili Saga lilivyokaa kama Hali ya mambo itaendelea hivi yeye ndiye atakayeangushiwa jumba bovu. Kimfumo lipo hivyo kwa lazima ajihami zaidi.

8. Sioni sababu ya viongozi kushinda kwenye Media kuendelea kutoa ufafanuzi badala yake waje na Solutions. Kwamba tumesikia vilio vyenu watanzania, Serikali hii ni ya kwenu tumekuja na plan A,B,C,D. Sio kung'ang'ania hapo hapo tu. Kazi ya Serikali ni kupunguza malalamiko Kwa wananchi..... 

Tuijenge nchi yetu kwa Pamoja na tulipende Taifa letu.

Ole Mushi
0712702602.


"New beginning starts here at brightermango. We make your day, brightens it and inspire your night"~GWEMELA

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post