![]() |
Pikipiki 12 kwa watendaji wa kata za |
PICHA: Mkurugenzi wa Mji wa Kasulu, mkoa wa Kigoma bi: Fatna Laay amekataa kutumia fedha zote shilingi milioni 210 alizopewa kwa ajili ya kujinunulia gari lake la kazi na badala yake ameigawanya fedha hiyo na kuwanunulia Pikipiki Watendaji wa Kata 12 waliomo kwenye mji huo
Maamuzi ya kupatiwa fedha hizo milioni 210 ilitokana na Mkurugenzi huyo kutumia gari bovu kwa miaka mitatu ambapo baada ya kupewa fedha hizo aliamua kununua gari la milioni 162 huku fedha zilizobaki ambazo ni milioni 47 akinunua Pikipiki 12 kwa Watendaji wa Kata 12 na amezikabidhi leo kwa kushirikiana na Mbunge wa Kasulu Mjini ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako.
Je ingewezekana kwako wewe kiruhusu pesa ile ikawe msaada kwa watendaji wa kata.