NEY WA MITEGO AAHIDI KUACHA "MAUZO" " SHOW OFF" AU "KUJIONYESHA"

Baada ya kugundua kuwa... yeye bila mashabiki sio kitu... aahidi kutoishi kwa kuonyesha sana utajiri wake wazi wazi kwa watu wanaomsaupport ilhali akijua hawana mali au vitu anavyovionyesha.

Nay wa Mitego ajuta "Sitaki kujionyesha tena"

Nay wa Mitego amesema amejifunza mambo mengi hivyo hataki kuyaonyesha maisha yake kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo akifanya 'show off' za mali zake kama gari, nyumba  au hata mpenzi wake.
Nay wa Mitego akiwa nyumbani kwake.



Msanii huyo amesema hivyo kwa sababu anaamini mashabiki wake wengi ni wale wa hali ya chini na wa mtaani hivyo hataki kuwaumiza roho kwani bado anahitaji sapoti yao kwenye shughuli zake za kimuziki.

"Sitaki kujionyesha tena watu wanajua kama nafanya muziki sipendi ku-show off, watu wanaonisapoti kula yao ni shida lakini wananipenda, mashabiki wangu wengi asilimia kubwa ni walala hoi, watafutaji, wamachinga wanamaisha ya kuungaunga sitaki kuwaumiza roho bado nahitaji sapoti yao" ameeleza Nay wa Mitego.

"New beginning starts here at brightermango. We make your day, brightens it and inspire your night"~GWEMELA

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post