Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade) imesaini hati ya makubaliano ya TZS Milioni 420 na benki ya NBC kwa ajili ya ujenzi wa sanamu la aliyekua Rais wa 5 wa Tanzania, John Pombe Magufuli katika viwanja vya maonesho ya biashara (Sabasaba) jijini Dar.
Pamoja na sanamu hilo, pesa hizo pia zitakarabati baadhi ya kumbi katika viwanja hivyo kwa viwango vya kisasa. Mkurugenzi wa TanTrade, Rutageruka Sabi amesema ujenzi wa sanamu hilo umelenga kuenzi jitihada na mchango wa Magufuli katika kuinua uchumi wa viwanda.
![]() |
Hayati Dr Magufuli. |
"New beginning starts here at brightermango. We make your day, brightens it and inspire your night"~GWEMELA