Mahakama inayotajwa kuwa ya juu zaidi Nchini Afrika Kusini imekubali kusikiliza ombi la kukata rufaa lililotolewa la kuifuta hukumu ya miezi 15 jela iliyotolewa kwa Rais wa zamani wa Nchi hiyo Jacob Zuma.
Hii ni baada ya Mahakama kumuhukumu miezi 15 jela wiki hii kwa kosa la kudharau na kupuuza amri ya Mahakama ya kumtaka kufika mbele ya Tume maalumu inayochunguza madai mbalimbali ya rushwa dhidi yake wakati alipokua madarakani 2009-2018.
Mitandao ya Afrika Kusini leo imeripoti kwamba Mahakama imekubali ombi la Zuma kukata rufaa kupinga hukumu hiyo…. Zuma alikua Rais kwa miaka 9 lakini alijiuzulu Urais February 2018 kutokana na kushutumiwa kwa ufisadi, uchumi na umaarufu wa Nchi kushuka huku shinikizo kubwa likitoka kwa Chama chake cha ANC kilichotishia kumuondoa kwa kura ya Bunge ya kutokuwa na imani nae iwapo hatojiuzulu.
Raisi wa zamani wa South Africa; Jacob Zuma. |
From Milardayo.updates
"New beginning starts here at brightermango. We make your day, brightens it and inspire your night"~GWEMELA