#MICHEZO UJASIRI WA #OLIVIER GIROUD NA MAAJABU YA USIKU WA ULAYA #UEFA

Image by gettyimages

 Na brightermango.

Kutokana na kuwepo kwa Tammy Abraham, Olivier Giroud ameonekana kuwa chaguo la pili kwa meneja wake Frank Lampard.


Pasipo na kinyongo Giroud amekua akifanya vizuri na Timu yake ya taifa na kwa upande wa vilabu akiwa na ubora hasa kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya.


MAAJABU YA GIROUD.

Hata kama kwa kiasi fulani amekuwa akikosa nafasi timu ya kwanza kwenye machaguo ya Meneja wake, bado Giroud hajaacha kabisa kuwa kiranja mkuu kwenye vyumba vya kubadilishana nguo na kwenye mazoezi, iliarifu tovuti ya bbc.com.


Kwa upande mwingine Kocha nae amesifu usaidizi wa Giroud kwenye mashindano yote, yale ya ligi kuu na hata yale ya kimataifa.



UJASIRI WAKE GIROUD.


Giroud mwenye ushindi wa kombe la dunia akiwa na taifa la ufaransa kwa sasa ndio Mshambuliaji pekee anaendelea kucheza akiwa na magoli mengi kitaifa na akiwa ni wa pili kitaifa ukimtoa tu Thiery Henry.

Pia Giroud amefunga magoli manne kwenye mechi ya Uefa hapo jana usiku, hii ikimaanisha kuwa Giroud hajakata tamaa bali anazidi kuwa na ujasiri wa kufanya zaidi.

 We believe, life is only a gift that expires and success in anything we have is not ours, its for human kind and so our wisdom'' -Gwemela

Post a Comment

THANK YOU FOR A COMMENT!

Previous Post Next Post